Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-EU-Usalama

Kikosi cha wanajeshi kutoka EU chasubiriwa jamhuri ya Afrika ya Kati

Mapigano mapya ya kidini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesabisha vifo vya watu 30 wakati huu wanajeshi kutoka Umoja wa ulaya wakiwasili nchini humo kulinda amani. Kikosi cha askari polisi wa Ufaransa, nchi pekee barani Ulaya ambayo ina wanajeshi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wameanza kupiga doria katika mji mkuu wa nchi hio Bangui, katika hali ya kusubiri uamzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kukituma kikosi cha wanajeshi 12 000.

Wanajeshi wa Ufaransa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui.
Wanajeshi wa Ufaransa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Hayo yakijiri wanajeshi wawili wa Ufaransa wamejeruhiwa jana mjini Bangui, baada ya kurushiwa gruneti na mtu waliyokua wakimshikiliya, amefahamisha kanali François Guillermet, ambaye anahusika na mawasiliano katika kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

“wanajeshi wetu wamekua wakimkagua mtu ambaye amekua amelewa, ambaye amekua na silaha, na wakati aliporusha gruneti, iliwajeruhi papo hapo watu wawili”, amesema afisa huyo.

Baada ya kuwasili, wanajeshi hao 55 wamenza Operesheni jijini Bangui katika juhudi za kulinda amani chini ya kivuli cha Umoja wa Ulaya (Eufor).

Wanajeshi hao wamekua wakipewa mafunzo na wanajeshi wa Ufaransa waliyokutwa nchini Jamhuri ra Afrika ya Kati katika operesheni Sangaris.

Wachambuzi wa siasa za Kimataifa na mizozo wanasema hatua hii ya Umoja wa Mataifa imechelewa.

Polisi hao 55 wameanza kupiga doria katika baadhi ya mitaa ya Bangui ambako kumekua kukishuhudiwa machafuko kama vile mtaa wa PK5, ambako waislamu wengi waliuliwa na wanamgambo wa kundi la anti-balaka.

Operesheni ya wanajeshi 800 kutoka Umoja wa Ulaya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo ilitangazwa aprili 1, itaanza shughuli yake mwishoni mwa mwezi mei, amesema Philippe Pontiès, afisa wa ngazi ya katika jeshi la Ufaransa, ambaye pia ataongoza kikosi hicho cha wanajeshi kutoka Umoja wa Ulaya.

Kikosi hicho kitakua na majukumu ya kulinda uwanja wa ndege na baadhi ya mitaa ya mji wa Bangui, ambako mauaji yalikomeshwa tangu wanajeshi wa Ufaransa walipo ingia mjini humo, hata kama bado kuna shuhudiwa mara kwa mara machafuko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.