Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-UE-Usalama

Umoja wa Ulaya watangaza kuanza operesheni zake za kijeshi nchini Jamhuri ya Afrika ya kati

Umoja wa Ulaya umeanzisha operesheni ya kijeshi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, baada ya kuaanda miezi kadhaa zoezi la kukusanya wanajeshi wanaohitajika, hayo ni wakati taifa hilo linakutana linakabiliwa na machafuko.

Umoja wa Ulaya umeidhinisha kikosi cha wanajeshi 1000 kusaidia wanajeshi wa Ufaransa (picha) na wale Umoja wa Afrikanchini Afrika ya Kati.
Umoja wa Ulaya umeidhinisha kikosi cha wanajeshi 1000 kusaidia wanajeshi wa Ufaransa (picha) na wale Umoja wa Afrikanchini Afrika ya Kati. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Umoja wa Ulaya limeanzisha operesheni hio ya kijeshi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ili kuchangia katika kurejesha hali ya utulivu katika taifa hilo, ambalo kwa mujibu wa tangazo liliyotolewa na baraza hilo, “linakabiliwa na machafuko ya kidini”.

“Kikosi hicho kitaundwa na wanajeshi 1000, na kitaongozwa na kiongozi wa kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa, Philippe Pontiès”, Baraza la Umoja wa Ulaya limefahamisha.

Ufaransa, ambayo ina wanajeshi wake wapatao 2000, iliomba ukisisitiza tangu awali kwamba kikosi hicho kutoka bara la Ulaya kishirikiane na kikosi cha wanajeshi kutoka Umoja wa Afrika Misca.

Lakini kikosi hicho kitakua na kazi ya kulinda uwanja wa ndege na baadhi ya mitaa ya mji wa Bangui, na itachukua muda wa kukituma nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, amesema mmoja wa mabalozi kutoka Ulaya.

Tangazo hilo linatolewa mkesha wa mkutano kuhusu Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao unatazamiwa kufunguliwa leo mjini Brussels, ambao ni mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na viongozi wa mataifa ya bara la Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.