Pata taarifa kuu
Australia-Kampeni

Australia yalaumiwa kukataa kuwpaokea wakimbizi kwa kisisngizio cha kupambana na wahamiaji haramu

Australia imeingia matatani baada ya kutuhumiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu kutokana na hatua yake ya kukataa Kundi la Wakimbizi kutoka nchi za Sri Lanka, Myanmar na Kuwait kwa kisingizio cha kuendelea mapambano dhidi ya wahamiaji haramu.

Bango la kampeni ya uchaguzi wa Septemba 7, 2013 waziri mkuu Kevin Rudd (kushoto) na kiongozi wa upinzani Tony Abbott (Kulia).
Bango la kampeni ya uchaguzi wa Septemba 7, 2013 waziri mkuu Kevin Rudd (kushoto) na kiongozi wa upinzani Tony Abbott (Kulia). REUTERS/Daniel Munoz
Matangazo ya kibiashara

Tuhuma hizi za Shirika la Kutetea Haki za Binadamu linakuja kipindi hiki kampeni za Uchaguzi Mkuu zikiendelea kupambana moto huku sera ya kukabiliana na uhamiaji haramu ikiwa ni moja ya suala linalogonga vichwa vya wananchi wengi.

Waziri Mkuu anayetetea wadhifa wake Kevin Rudd kwenye kampeni zake ameendelea kuweka bayana hawatakuwa tayari kuendelea kuwa kituo cha kufanyika kwa biashara za binadamu pamoja na kuwahifadhi mamia ya wahamiaji haramu.

Kiongozi wa Upinzani ambaye anausaka kwa udi na uvumba Uwaziri Mkuu nchini Australia Tonny Abbot amesema huu ni wakati mzuri wa kupitia sera hiyo ya uhamiaji ili kuhakikisha wanajenga uhusiano mzuri na mataifa jirani.

Wananchi wa Australia wanatarajiwa kupiga kura tarehe saba ya mwezi Septemba kuchagua Serikali mpya ambayo itaongoza na Chama kitakachokuwa na wabunge wengi ndicho kitatoa Waziri Mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.