Pata taarifa kuu
LONDON

Mexico yaiachakaza Brazil fainali za Olyimpiki.

Timu ya soka ya Mexico imewastaajabisha mashabiki wa mchezo huo kwa kuichapa timu ya soka ya Brazil kwa magoli 2-1 kwenye fainali ya Kombe la Olimpiki katika uwanja wa Wembley mjini London. 

Goli la kwanza la Mexico likiingia nyavuni mwa Brazil
Goli la kwanza la Mexico likiingia nyavuni mwa Brazil latinospost.com
Matangazo ya kibiashara

Mexico ilipata bao lake la kwanza katika sekunde ya 29 baada ya kipenga cha kuanza mchuano kupulizwa, kupitia kwa mshambuliaji wake Oribe Peralta ambapo hadi kipindi cha kwanza kumalizika Mexico iliongoza kwa bao1 Brazil ikiwa haina kitu.

Hili ni bao la kwanza kufungwa haraka zaidi katika kipindi cha miaka 36 ya mashindano ya soka ya Olimpiki.

Kwa mara nyingine mshambuliaji huyo huyo alirudi kutikisa nyavu za Brazil mnamo dakika ya 75 kwa mpira wa kichwa.

Nayo Brazil ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa mshambuliaji Givaldino Hulk, zikiwa zimesalia dakika chache kumalizika kwa mchezo.

Hadi kipenga cha mwisho Mexico 2 Brazil 1.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.