Pata taarifa kuu
TANZANIA-ZANZIBAR

Hakuna matumaini ya kuwapata manusura zaidi visiwani Zanzibar

Waokoaji visiwani Zanzibar nchini Tanzania wanasema wamekataa tamaa kuwapata zaidi ya watu 80 ambao hawajulikani walipo baada ya kuzama kwa meli ya abiria siku ya Jumatano barani Hindi .

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu 60 akiwemo mtalii mmoja wa kigeni wamefariki na wengine 146 kuokolewa wakiwa hai kutokana na ajali hiyo ya meli ya abiria iliyokuwa na abiria 291 kutoka Dar es salaam kwenda Zanzibar.

Msemaji wa jeshi la polisi visiwani Zanzibar Mohamed Mhina anasema matumaini ya kuwapata manusura zaidi wakiwa hai yalididimia siku ya Alhamisi baada ya meli hiyo kuzama zaidi majini.

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amezuru Zanzibar na kutaka uchunguzi kufanyika ili kubaini kiini cha ajali hiyo .

Tanzania inaomboleza siku tatu za mkasa huo ambao umetokea baada ya meli nyingine kuzama mwezi Septemba mwaka 2011 na kusababisha kufariki kwa zaidi ya abiria 200.

Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kuthibiti usalama wa vyombo vya usafiri majini kutokana na ongezeko la  ajali za meli ya abiria ambazo zimeongezeka katika siku za hivi karibuni.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.