Pata taarifa kuu
KIGALI-RWANDA

Rwanda yazifunga mahakama za kijadi za 'Gacaca' zilizokuwa zinashughulikia mauaji ya mwaka 1994

Serikali ya Rwanda hapo jana imetangaza kuzifunga rasmi mahakama za kijadi za 'Gacaca" zilizokuwa zimefunguliwa kwaajili ya kusikiliza kesi za watuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 yaliyotokea nchini humo.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Rais wa Rwanda, Paul Kagame Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa kufungwa kwa mahakama hizo ulitangazwa na rais Paul Kagame mjini Kigali ambapo amekiri kuwa kwa kiasi kikubwa mahakama hizo zilisaidia kuleta utangamano miongoni mwa wananchi wa Rwanda.

Toka kufunguliwa kwa mahakama hizo mwaka 2001 zimeweza kutoa huku kwa watu zaidi ya asilimia 65 ambao walikuwa wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki yaliyotokea nchini humo.

Mahakama hizo zilizokuwa zaidi elfi kumi na mbili na mia moja zilikuwa zikitumia viongozi wa kijadi katika kutoa hukumu kwa watu ambao walikuwa wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mwaka 1994.

Licha ya kufungwa kwa mahakama hizo, kumekuwa na ukosolewaji mkubwa kuhusu utendaji kazi wa mahakama zenyewe katika kutenda haki kwa watu ambao walikuwa wakishtakiwa kwenye mahakama hizo.

Mwaka jana amshirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo yalitoa ripoti kuonyesha ukiukwaji mkubwa wa sheria uliokuwa ukifanywa na wazee waliokuwa wakisikiliza kesi hizo.

Hatua ya kufungwa kwa mahakama hizo umekuja baada ya kuundwa kwa mahakama maalumu ya kushughulikia kesi za Rwanda ya ICTR iliyoko mjini Arusha Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.