Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-MAREKANI

Mwanajeshi wa Marekani aua raia wa Afghanstan

Raia kumi na tano wa Afghanstan wameuawa baada ya mwanajeshi wa Marekani kuwafyatulia risasi wakiwa katika makazi yao mapema jumapili vyanzo kutoka Afghanstan vimethibitisha.

Baadhi ya wanajeshi wa Marekani waliopo Afghanstan
Baadhi ya wanajeshi wa Marekani waliopo Afghanstan REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mwanajeshi wa Marekani anayetuhumiwa kutekeleza mauaji hayo anashikiliwa na majeshi ya kujihami ya NATO huko jimbo la Kandahar.

Shuhuda mmoja kutoka kijiji cha Najeeban katika wilaya ya Panjwayi Haji Samad, amesema kuwa mpaka sasa ndugu zake kumi na moja wameuawa.

Naye msemaji wa gavana wa jimbo hilo,Ahmad Jawed Faysal, amesema kuwa zaidi ya watu nane walipoteza maisha baada ya mwanajeshi huyo kuanza kufyatua risasi mapema asubuhi ya jumapili.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.