Pata taarifa kuu
MISRI-MAREKANI-PAKISTAN

Kiongozi wa Al Qaeda Seif Al Adel akamatwa Uwanja wa Ndege wa Cairo Nchini Misri

Kiongozi wa Kundi la Mtandao la Al Qaeda Seif Al Adel ambaye anasakwa kwa udi na uvumba kutokana na kupanga na kutekeleza mashambulizi ya mabomu kwenye Balozi za Marekani mwaka 1998 amekamatwa katika Uwanja wa Ndege nchini Misri.

Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Seif Al Adel ambaye amekuwa akitafutwa tangu mwaka 1998 kwa kitita cha dola milioni 5
Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Seif Al Adel ambaye amekuwa akitafutwa tangu mwaka 1998 kwa kitita cha dola milioni 5
Matangazo ya kibiashara

Al Adel amekamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Cairo akiwa anatokea nchini Pakistan ambapo kabla ya hapo alitua Dubai kabla ya kuendelea na safari yake kabla ya kukamatwa huko Cairo na vyombo vya usalama.

Polisi nchini Misri imefanikiwa kumkamata Al Adel ambaye anatajwa kutekeleza mashambulizi nchini Tanzania Kenya kwenye Balozi za Marekani baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Cairo.

Televisheni ya Taifa nchini Misri ndiyo ilikuwa ya kwanza kutangaza habari za kukamatwa kwa Al Adel ambaye amekuwa akisakwa bila ya mafanikio yoyote tangu mwaka elfu moa mia kenda tisini na nane.

Mzaliwa huyo wa Misri ambaye anatambulika kwa jina la Mohammad Ibrahim Makkawi alikuwa ni miongoni mwa walinzi wa Kiongozi wa Mtandao wa Al Qaeda Dunian Marehemu Osama Bin Laden aliyeuawa nchini Pakistan.

Al Adel aliondolewa kwenye kikosi cha Ulinzi wa Osama Bin Laden kabla ya kifo cha Kiongozi huyo ambapo sasa nafasi yake kwa sasa inashikiliwa na Msaidizi wake Mohammed Al Zawahiri.

Al Adel ambaye alikuwa kwenye orodha ya watu wanaotafutwa ya Polisi wa Marekani FBI huku zawadi ya kukamatwa kwake ikiwa ni dola milioni tano amekamtwa akiwa kwenye shughuli zake za kawaida.

Taarifa zilikuwa zinamhusisha Al Adel kukimbilia nchini Iran kutokana na Majeshi ya Marekani kufanya uvamizi nchini Afghanistan mwaka 2011 pamoja na Mtoto wa Osama, Saad Bin Laden.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.