Pata taarifa kuu

Watu saba wamefariki katika tetemeko la ardhi nchini Taiwan

Nairobi – Karibia watu saba wamefariki katika tetemeko la ardhi nchini Taiwan wakati wengine zaidi ya 700 wakiripotiwa kujeruhiwa, majengo kadhaa pia yakiharibiwa.

Zaidi ya watu 700 wameripotiwa kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi nchini Taiwan.
Zaidi ya watu 700 wameripotiwa kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi nchini Taiwan. AFP - WAY
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mamlaka kwenye taifa hilo, hili ndilo tetemeko kubwa zaidi la ardhi lenya uzito wa 7.4 kuwatokea katika kipindi cha miaka 25.

Mwaka wa 1999, watu karibia 2,400 waliripotiwa kufariki katika tetemeko lengine la ardhi lenye uzito wa 7.6, tukio ambalo lilitajwa kuwa mbaya zaidi katika historia ya kisiwa hicho.

Idara ya wazima moto nchini humo imesema watu waliofariki wanatoka katika eneo la Hualien, watu wengine 736 wakithibitishwa kujeruhiwa.

Watu saba wamethibitishwa kufariki katika mkasa huo.
Watu saba wamethibitishwa kufariki katika mkasa huo. via REUTERS - TAIWAN NATIONAL FIRE AGENCY

Picha zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zimeonyesha majengo yalioharibiwa na tetemeko hilo.

Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida, nchi jirani na Taiwan, kupitia mtandao wake wa X zamani ukiitwa Twitter amesema kuwa nchi yake itaipa Taiwan msaada unaohitajika wakati huu ambapo imekabiliwa na tetemeko kubwa la ardhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.