Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

India: Upinzani waandamana baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa New Delhi

Upinzani umeandamana nchini India, siku kumi baada ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa New Delhi. Umati mkubwa ulikusanyika katika mji mkuu siku ya Jumapili kwa mwito wa vyama vikuu vya upinzani. Wakati uchaguzi ukitarajiwa kunaanza Aprili 19, wamesisitiza kwamba hawatasalimu amri kwa vitisho vya kukamatwa au kufungwa.

Wafuasi wa chama cha Aam Aadmi Party (AAP) wakati wa maandamano yalioandaliwa na upinzani huko New Delhi, Machi 31, 2024.
Wafuasi wa chama cha Aam Aadmi Party (AAP) wakati wa maandamano yalioandaliwa na upinzani huko New Delhi, Machi 31, 2024. © Manish Swarup / AP
Matangazo ya kibiashara

Tangu kuanza kwa mwaka 2024, upinzani wa India unasema umenyanyaswa kuliko hapo awali. Mawaziri wakuu wawili wa majimbo yanayotawaliwa na upinzani walikamatwa bila kesi na akaunti za benki za chama cha Congress zilifungwa. Hivyo, viongozi wa upinzani nchini India walikusanyika siku ya Jumapili na maelfu ya wafuasi wao katika mji mkuu New Delhi kupinga.

Aparna, 33, alihudhuria maandamano haya na mumewe. “Nilikuwa mwanaharakati wa kisiasa miaka 5 iliyopita na ninakuwa mmoja tena katika hali ya dharura. Sisi sote tuna wasiwasi sana kuhusu kile kinachotokea nchini India. Katikati ya uchaguzi, serikali inataka kuwanyamazisha wapinzani wake wote wa kisiasa. Maandamano kama hayo inanipa matumaini kwamba India na Wahindi wataendelea kupambana dhidi ya utawala huu mbovu,” anasema.

Kukamatwa kwa kiongozi wake Arvind Kejriwal, kinara wa kisiasa, leo ni kiini cha hotuba za vyama vyote vilivyokuja kudai kuachiliwa kwake na kuonyesha umoja wao. Kando ya AAP, takwimu kutoka chama cha Congress, wakomunisti na vyama vya kikanda TMC au DMK walipishana ukumbini wakiwahotubia wafuasi wao, huhu awakipiga makofi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.