Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-ULINZI

Urusi: Kim Jong-un na Vladimir Putin wakutana Vostotchny cosmodrome

Rais wa Urusi Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamekutana katika ukumbi wa Urusi wa Vostochny mashariki mwa Urusi. Kim Jong-un na Vladimir Putin watafanya mazungumzo kuhusu "mahusiano ya kibiashara" na "mambo ya kimataifa" katika kituo cha kurushia vyombo vya anga, mashirika ya habari ya Urusi yameripoti.

Urusi, Vostochny cosmodrome, Septemba 13, 2023: Rais wa Urusi Vladimir Putin akimkaribisha mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Urusi, Vostochny cosmodrome, Septemba 13, 2023: Rais wa Urusi Vladimir Putin akimkaribisha mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. via REUTERS - SPUTNIK
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un amewasili katika ukumbi wa Vostochny Cosmodrome mashariki mwa Urusi, ambapo Rais wa Urusi Vladimir Putin yuko. Mkutano wa viongozi hao wawili unaweza kupelekea, kwa mujibu wa Washington, kufikia makubaliano ya uuzaji wa silaha ili kusaidia mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wamewasili katika ukumbi wa Vostochny Cosmodrome mashariki mwa Urusi, mashirika ya habari ya Urusi yalitangaza Jumatano. Katika mchakato huo, Vladimir Putin alitangaza kuwa Urusi itaisaidia Korea Kaskazini kutengeneza satelaiti, tena kwa mujibu wa mashirika ya Urusi.

Vladimir Putin na Kim Jong-Un watazungumzia kuhusu "masuala nyeti", kulingana na msemaji wa Kremlin Dmitri Peskov.

Akiwasili nchini Urusi Jumanne jioni, Kim Jong-un anafanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuanza kwa janga la UVIKO-19. Tayari alikuwa amekutana na Vladimir Putin wakati wa safari yake ya awali nje ya nchi, huko Vladivostok mwaka wa 2019. Mahali na tarehe ya mkutano wao, Jumatano hii, vilivuja hivi punde, katika saa za mwisho.

'Jambo muhimu kwetu ni maslahi ya nchi zetu'

Washington inahofia kwamba Urusi itapata silaha kwa ajili ya operesheni zake za kijeshi nchini Ukraine kutoka Korea Kaskazini, yenyewe ambayo inakabiliwa na vikwazo kwa sababu ya mipango yake ya nyuklia na makombora.

"Katika kujenga uhusiano wetu na majirani zetu, ikiwa ni pamoja na Korea Kaskazini, jambo muhimu kwetu ni maslahi ya nchi zetu na si maonyo kutoka Washington," amesema Dmitri Peskov.

Kim Jong-un ameandamana na maafisa wakuu wa kijeshi, akiwemo waziri wake wa ulinzi na maafisa kutoka vyombo vya uzalishaji silaha na sekta ya teknolojia ya anga, kulingana na vyombo vya habari vya serikali hizi mbili.

Kulingana na wataalamu, mkutano kati ya Vladimir Putin na Kim Jong-un unaweza kuzingatia makubaliano katika uwanja wa silaha, kwa sababu Vladimir Putin anatafuta kupata makombora ziada na makombora yanayoangamiza vifaru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.