Pata taarifa kuu

Iran:Watu sita wakamatwa kwa kupanga ghasia kuelekea kumbukumbu ya kifo cha Mahsa Amini

Nairobi – Mamlaka katika eneo la kusini-magharibi mwa Iran imewakamata watu sita wanaotuhumiwa kupanga ghasia katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kifo cha Mahsa Amini kizuizini ambacho kilisababisha maandamano nchini kote, vyombo vya habari vya serikali viliripoti leo.

Raia nchini Iran  waandamna kufuatia kifoo chake Mahsa Amini mwaka jana
Raia nchini Iran waandamna kufuatia kifoo chake Mahsa Amini mwaka jana © @Reuters
Matangazo ya kibiashara

Amini, ambaye alikuwa Mkurdi wa Irani, alikufa mnamo Septemba 16, 2022, baada ya kukamatwa huko Tehran kwa madai ya kukiuka sheria kali za jamhuri ya Kiislamu ya mavazi kwa wanawake.

Shirika la kijasusi la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika mkoa wa Kohgiluyeh na Boyerahmad ilifunga kurasa tano za mitandao ya kijamii na kuwakamata watu sita walioukuwa wanaendesha taarifa za uchochezi.Hii ni kulingana na shirika rasmi la habari la IRNA.

Shirika la kijasusi la IRGC liliwashutumu washukiwa kwa kuandaa ghasia na kuchochea usalama  mbaya kupitia  mtandao, na kuongeza kuwa kulikuwepo na rekodi za uhalifu zinazowahusisha.

Maandamano kote Iran katika miezi iliyofuata kifo cha Amini yalishuhudia mamia ya watu wakiuawa, wakiwemo makumi ya maafisa wa usalama, na maelfu kukamatwa kuhusiana na kile maafisa walichokiita "machafuko" yaliyochochewa na wageni.

Kukamatwa kwa hivi punde kumekuja siku chache baada ya shirika la kijasusi la IRGC na wizara ya ujasusi ya Tehran kutangaza kuwa wametambua kinachoendelea mitandaoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.