Pata taarifa kuu

Waziri wa Biashara wa Marekani azuru China katikati ya hali ya mvutano

Waziri wa Biashara wa Marekani Gina Raimondo anasafiri hadi Beijing na Shanghai Jumapili hii, Agosti 27 kukutana na maafisa wakuu wa China. Ziara ya siku nne ambayo inatarajiwa kukamilika Jumatano. Safari yenye umuhimu mkubwa huku uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukiwa bado haujakamilika kutokana na masuala mengi, kutoka Taiwan hadi Bahari ya China, ikiwa ni pamoja na biashara bila shaka.

Waziri wa Biashara wa Marekani Gina Raimondo.
Waziri wa Biashara wa Marekani Gina Raimondo. REUTERS - KEVIN LAMARQUE
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa ziara yake nchini China, Gina Raimondo atalazimika kutumia diplomasia, kwa sababu misheni yake ni tete kwa kiasi fulani. Waziri wa Biashara wa Marekani atajaribu ktekeleza kazi yake ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Beijing kwani Washington imeweka vikwazo kadhaa kwa mauzo yake ya nje kwenda China. Vikwazo vilivyowekwa na wizara inayoongozwa na Gina Raimond, anakumbusha mwandishi wetu wa New York, Loubna Anaki. Kwa hiyo dhamira ya Gina Raimondo ni kuwashawishi Wachina na Wamarekani kwamba inawezekana kuwa na mahusiano ya kibiashara huku wakiweka mipaka ya "kulinda" maslahi ya Marekani. Akiwa na ujumbe wa wafanyabiashara wa Marekani, Waziri wa Biashara anatarajiwa kukutana na mwenzake wa China pamoja na maafisa wengine wakuu nchini humo.

Mkakati wa kufufua viwanda

Vyombo vya habari vya Marekani vinamzungumzia gavana wa zamani wa Rhode Island, ambaye alianza kazi yake ya kifedha, matarajio huko Washington. Kilicho hakika ni kwamba ushawishi wake tayari unasikika katika siasa za utawala wa Marekani tangu Joe Biden alipomsajili kushiriki katika mchakato wa kuweka sawa sekta ya viwanda nchini. Na ili tasnia ya Marekani iweze kuwa na ushindani tena, Gina Raimondo ameamua kukatisha ufikiaji wa kampuni za China kwa teknolojia ya hali ya juu zaidi: hii ndiyo sababu sekretarieti yake imeweka orodha nyeusi ya kampuni na bidhaa nyeti ambazo sasa ilikuwa marufuku kufanya biashara na Beijing.

Kama Wazungu, Wamarekani wanawekeza kwa kiasi kikubwa kuhamisha utengenezaji wa vichakataji vidogo, chip ambazo ni muhimu kwa kila kitu kinachohusisha kompyuta. Shida ndogo, ikiwa China iko nyuma kwenye teknolojia, inadhibiti idadi kubwa ya ardhi adimu muhimu kwa utengenezaji wa vichakataji vidogo. 

Maendeleo yanayotarajiwa

Ziara ya Gina Raimondo ni ya nne ya mjumbe wa utawala wa Biden katika miezi ya hivi karibuni, uthibitisho wa umuhimu uliotolewa na rais wa Marekani kwa uhusiano na Beijing, ambao umedorora kutokana na masuala mengi wanaotofautiana. Huko Washington, baadhi wanatumai kuwa ziara hii itataleta maendeleo madhubuti zaidi kuliko wakati wa ziara za maafisa wa zamani wa Marekani. Miezi michache kabla ya mkutano uliopangwa kufanyika mwezi Novemba kati ya Xi Jinping na Joe Biden, Gina Raimondo kwa hiyo anajiandaa kwa kazi ngumu ya kusawazisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.