Pata taarifa kuu

Marekani: Joe Biden aiita China 'bomu linalotarajia kulipuka'

Wakati wa ziara yake huko Utah, rais wa Marekani ameelezea mgogoro wa kiuchumi unaoikumba China ambayo inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi baada ya idadi kubwa ya wafanyakazi kuonekana kuzeeka.

Le président américain Joe Biden prononce un discMwishoni mwa mwezi Juni, rais Joe Biden aliiudhi Beijing kwa kuzingatia kwamba mwenzake Xi Jinping ni kutoka kundi la "madikteta", maoni yalichukuliwa na diplomasia ya China kama "uchochezi".
Le président américain Joe Biden prononce un discMwishoni mwa mwezi Juni, rais Joe Biden aliiudhi Beijing kwa kuzingatia kwamba mwenzake Xi Jinping ni kutoka kundi la "madikteta", maoni yalichukuliwa na diplomasia ya China kama "uchochezi". REUTERS - KEVIN LAMARQUE
Matangazo ya kibiashara

Hii ni kauli ambayo haijaifurahisha Beijing. Siku ya alhamisi rais wa Marekani Joe Biden alisema kwamba hasimu mkuu wa Marekani China ni "bomu linalotarajia kulipuka kwa njia nyingi", akitaja matatizo yake ya kiuchumi na nguvu kazi inayozeeka.

Wakati wa ziara yake huko Utah, magharibi mwa Marekani, rais wa Joe Biden amesema kuwa China inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa ajira na kwamba wafanyakazi wake wanazeeka. Kwa sababu hii, nchi hii "iko katika matatizo", amesema. Kwa mujibu wa Joe Biden, hii inatoa sababu ya kuwa na wasiwasi kwani, "wakati watu wabaya wanakabiliwa na shida, hufanya mambo mabaya".

Biden haitakii 'china mabaya'

Mwishoni mwa mwezi Juni, rais Joe Biden aliiudhi Beijing kwa kuzingatia kwamba mwenzake Xi Jinping ni kutoka kundi la "madikteta", maoni yalichukuliwa na diplomasia ya China kama "uchochezi". Siku ya Alhamisi, hata hivyo, Joe Biden alihakikisha kwamba alikuwa akitafuta kudumisha "uhusiano mzuri na China". "Siitakii mabaya yoyote China, lakini ninaangalia. "

Hivi majuzi Marekani ilizindua upya mazungumzo yake na China, kwa mfululizo wa ziara za maafisa wakuu wa Marekani mjini Beijing, akiwemo mkuu wa diplomasia Antony Blinken. Madhumuni ya ziara hii ni kufungua ukurasa kwenye kipindi cha hivi majuzi cha mvutano, kuhusiana na puto la China lililoelezwa kama la "kijasusi" ambalo lilidunguliwa na Marekani mwezi Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.