Pata taarifa kuu

Antony Blinken wa Marekani amefanya mazungumzo na rais Xi wa China

NAIROBI – Rais Xi Jinping wa China, wakati wa mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani anayezuru Beijing Antony Blinken, amesema nchi hizo  "zimepiga hatua" katika masuala kadhaa.

Beijing na Washington zinalenga kumaliza mvutano kati yake
Beijing na Washington zinalenga kumaliza mvutano kati yake © AP / Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza kuwahifanywa na afisa wa ngazi ya juu wa Marekani nchini katika kipindi cha miaka mitano, ziara inayokuja wakati huu pia uhusiano  kati ya Beijing na Washington ukionekana kudorora.

"Upande wa China umeweka wazi msimamo wetu na pande zote mbili zimekubaliana kufuata maelewano ya pamoja ambayo Rais Biden na mimi tulikuwa tumefikia huko Bali," Xi alimwambia mwanadiplomasia mkuu wa Marekani.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani na rais wa China Xi wamefanya mazungumzo jijini Beijing
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani na rais wa China Xi wamefanya mazungumzo jijini Beijing © AP / Leah Millis

"Pande mbili pia zimepiga hatua na kuafikia makubaliano juu ya baadhi ya masuala muhimu", aliongeza, bila kufafanua zaidi.

"Nina matumaini kuwa waziri  Blinken, kupitia ziara hii, anaweza kutoa mchango chanya kuimarisha uhusiano kati ya China na Marekani," aliongeza.

Mkutano huo ambao uliochukua zaidi ya nusu saa umefanyika  baada ya Blinken kufanya mazungumzo ya zaidi ya saa 10 kwa siku mbili na viongozi wengine wakuu nchini China.

Rais wa China Xi jinping amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken nchini humo
Rais wa China Xi jinping amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken nchini humo AP - Leah Millis

Awali,  Blinken alikuwa amekutana  na mkuu wa sera za kigeni wa China Wang Yi ambapo walifanya mazungumzo na wasaidizi wao, ambao tofauti na wakubwa wao walivalia barakoa kwa mujibu wa kanunzi za kudhibiti msambao wa  Uviko-19.

Kando na kikao cha mwaziri hao wa kigeni wa China na Marekani, Wang alimwambia Blinken kwamba safari yake "inakuja katika wakati muhimu kuhusu uhusiano wa China na Marekani", kulingana na shirika la utangazaji la serikali CCTV.

"Ni muhimu kufanya uwamuzi kati ya mazungumzo na makabiliano, ushirikiano au migogoro," alisema.

"Lazima tubadilishe mwelekeo wa kudorora kwa uhusiano kati ya China na Marekani, kushinikiza kurejea kwa njia yenye maelewano na utulivu, na kufanya kazi pamoja kutafuta njia sahihi kati ya China na Marekani kupatana," aliongeza Wang.

Pia alitoa onyo kuhusu  Taiwan, taifa linalojitawala kwa misingi ya kidemokrasia na ambalo Beijing inaliona kama sehemu ya ardhi yake.

Mwaka uliopita, China itekeleza mazoezi ya kijeshi  mara mbili karibu na kisiwa hicho baada ya kukasirishwa kutokana na mikutano kati ya wabunge wa ngazi ya juu wa Marekani na viongozi wa Taiwan.

Blinken kwa upande wake "alisisitiza umuhimu wa kusimamia  uwajibikaji katika ushindani kati ya Marekani na China kupitia njia wazi za mawasiliano ili kuhakikisha ushindani hausababishi migogoro,".

  

  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.