Pata taarifa kuu

India kutuma tena chombo chake cha anga za mbali cha Chandrayaan, Chandrayaan-3 mwezini

India inajiandaa kurusha roketi yake mwezini siku ya Jumatano, wakati wa kihistoria kwa nchi hiyo yenye watu wengi zaidi duniani ambayo inatarajia kujiunga na klabu ya kipekee ya wale waliofanikiwa kutua mwezini, miaka minne baada ya jaribio kama hilo kushindwa.

Picha ya skrini kutoka video ya Shirika la Utafiti wa Anga la India (ISRO) inayoonyesha kupaa kwa roketi isiyokuwa na rubani, Chandrayaan-3 (-), Julai 14, 2023.
Picha ya skrini kutoka video ya Shirika la Utafiti wa Anga la India (ISRO) inayoonyesha kupaa kwa roketi isiyokuwa na rubani, Chandrayaan-3 (-), Julai 14, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Chandrayaan-3 inatarajiwa kutua mwezini muda mfupi baada ya saa kumi na mbili jioni saa za India (sawa na nusu sa za Afrika ya Kati), karibu na ncha ya kusini ya mwezi, yaani upande wa giza wa Mwezi, ambao haujagunduliwa sana, jambo ambalo litakuwa la kwanza ulimwenguni kwa programu ya anga.

Hii ni sehemu ya mwezi ambapo hakuna chombo chochote ambacho kimewahi kufanikiwa kutua.

Jaribio hili jipya la programu ya India, kwa kasi kamili, linakuja miaka minne baada ya jaribio lingine kama hili kushindwa vibaya, timu ya iliyokuwa ardhini ilipoteza mawasiliano muda mfupi kabla ya kuwasili mwezini.

Chandrayaan-3 iliyotengenezwa na Shirika la Utafiti wa Anga la India (ISRO), inajumuisha moduli ya kutua iitwayo Vikram, inayomaanisha "shujaa" kwa Kisanskrit, na roboti ya rununu, inayoitwa Pragyan ("hekima" kwa Kisanskrit) ili kuchunguza uso wa Mwezi.

Misheni hii inafanyika siku chache baada ya Luna-25, kifaa cha kwanza kuzinduliwa na Urusi kwenda mwezini tangu mwaka 1976, kuanguka.

Chandrayaan-3, iliyozinduliwa wiki sita zilizopita, ilikwenda kwa mwendo wa kinyonga kufikia mwezini kuliko misheni ya Apollo ya Marekani ya miaka ya 1960 na 1970, ambayo ilifika mwezini kwa siku chache.

Roketi ya India kwa hakika haina nguvu zaidi kuliko Saturn V, roketi ya mpango wa mwezi wa Apollo wa Marekani. Ilibidi ifanye mizunguko mitano au sita ya duaradufu kuzunguka Dunia ili kupata kasi, kabla ya kutumwa kwa njia ya mwezi kwa kipindi cha mmoja.

Vikram ilijitenga na moduli yake ya mwendo wiki iliyopita na imekuwa akisambaza picha za uso wa Mwezi tangu iingie kwenye mzunguko wa mwezi Agosti 5.

Mkuu wa zamani wa anga za juu wa India, K. Sivan, anabaini kwamba picha za hivi punde zaidi zinazotumwa na ujumbe huo zinaonyesha kuwa hatua ya mwisho ya safari hiyo inapaswa kufaulu.

Lakini mbio za kwenda mwezini hazikuanza leo, zilianza miaka ya 1960. Wakati huo, kulikuwa na dau kati ya Marekani na Muungano wa Kisovieti kuhusu ni nani angekuwa wa kwanza kumpeleka binadamu mwezini.

Urusi ilishinda satelaiti ya kwanza katika mzunguko wa Dunia, mtu wa kwanza angani na kutua kwa chombo kisichokuwa na rubani kwenda mwezini, lakini kwa safari ya Apollo, Marekani alikuwa ya kwanza kutua mwezini na kupata mafanikio makubwa.

Mamilioni ya watu ulimwenguni kote walitazama mafanikio haya ya Marekani kwenye TV. Baadaye, Marekani ilituma vyombo kadhaa vilivyoongozwa na binadamu kwenda mwezini.

Mpango wa Apollo wa Marekani uliisha mnamo 1972.

Baada ya miongo mitano, hakuna nchi nyingine isipokuwa Marekani ambayo imefanikiwa kumpeleka binadamu mwezini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.