Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

China na Urusi kumarisha zaidi uhusiano wao wa kibiashara

Waziri Mkuu wa Urusi Mikhail Michoustin, ambaye anazuru China, Jumanne amepongeza uhusiano mkubwa kati ya nchi hizo mbili na kutarajia kuongezeka kwa biashara zao, kabla ya mkutano uliopangwa kufanyika Jumatano na Rais Xi Jinping.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov akiwa na waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi mjini Moscow.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov akiwa na waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi mjini Moscow. Reuters/Maxim Zmeyev
Matangazo ya kibiashara

 

"Urusi inathamini uhusiano wa karne nyingi na China," waziri mkuu amesema katika kongamano la kiuchumi huko Shanghai, kulingana na video iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi. "Nina uhakika kwamba mwaka huu tutafikia lengo lililowekwa na wakuu wa nchi Vladimir Putin na Xi Jinping la kuongeza biashara yetu hadi dola bilioni 200," ameongeza, akimaanisha takwimu iliyotangazwa katika mkutano wa Machi huko Moscow.

China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Urusi, na biashara kati ya nchi hizo mbili ilifikia rekodi ya juu - dola bilioni 190 - mnamo mwaka 2022, kulingana na data kutoka mamlaka ya Forodha ya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.