Pata taarifa kuu

Korea Kusini yafikiria kuipa silaha Ukraine

Tangu kuanza kwa vita, Seoul ilikuwa imesisitiza kupeleka tu misaada ya kibinadamu kwa Kyiv ili isiharibu uhusiano wake na Urusi. Lakini katika mahojiano na shirika la habari la Reuters, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol amesema atafikiria kupeleka silaha Ukraine ikiwa shambulio kubwa litatekelezwa dhidi ya raia.

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol akihojiwa na shirika la habari la Reuters ofisini kwake Seoul, Aprili 18, 2023.
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol akihojiwa na shirika la habari la Reuters ofisini kwake Seoul, Aprili 18, 2023. REUTERS - KIM HONG-JI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Seoul, Célio Fioretti

Mabadiliko ya mtazamo kwa vita vya Ukraine: ikiwa Korea Kusini hadi imechukuwa hatua fulani kwa kujitenga na vita vya Urusi nchini Ukraine, tangazo la Rais Yoon Suk-yeol linaweza kuwa hatua ya mabadiliko kwa vita hivi vinavyoendelea.

Kufikia sasa, Seoul haikutaka kuikasirishaMoscow kwa kuisaidia Ukraine kijeshi, hasa kwa sababu ya msaada ambao Vladimir Putin aliweza kuipa Pyongyang kama malipo. Kwa hivyo Korea Kusini iliridhika kuuza silaha zake kwa wanachama wa NATO, pamoja na Poland, jirani ya Urusi.

Katika tukio la 'mashambulizi makubwa kwa raia'

Hata hivyo, nyaraka za Pentagon zilizofichuliwa wiki iliyopita zinataja shinikizo la Marekani kwa Korea Kusini kupeleka silaha Ukraine. Korea Kusini iliombwa hasa msaada wa vifaa vya kuzuia mahambulizi ya angani na risasi.

Uungaji mkono wa kijeshi kwa Ukraine, anasisitiza rais wa Korea Kusini aliyehojiwa na shirika la habari la Reuters, uko chini ya masharti: "Ikiwa kungekuwa na hali ambayo jumuiya ya kimataifa isingeweza kuvumilia, kama vile mashambulizi makubwa dhidi ya raia, mauaji au ukiukaji mkubwa wa sheria za vita, inaweza kuwa vigumu kusisitiza kutoa tu msaada wa kibinadamu au kifedha,” amesema. Lakini ni vigumu kujua aliochotaka kusema Yoon Suk-yeol kwa maneno haya. Mada hiyo inaweza kujadiliwa wakati wa mkutano wake na Joe Biden katika Ikulu ya White mnamo Aprili 26 kusherehekea miaka 70 ya muungano kati ya nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.