Pata taarifa kuu

Rais Putin amezuru majimbo yaliochukuliwa kutoka kwa Ukraine

NAIROBI – Rais wa Urusi Vladimir Putin ametembelea majimbo ya Kherson na Lugansk nchini Ukraine, na kukutana na Makamanda wa jeshi la nchi yake katika eneo hilo. 

Rais wa Urusi Vladimir Putin amezuru majimbo yaliochukuliwa kutoka kwa Ukraine
Rais wa Urusi Vladimir Putin amezuru majimbo yaliochukuliwa kutoka kwa Ukraine via REUTERS - KREMLIN.RU
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Kremlin imethibitisha ziara hiyo ya rais Putin lakini, haikueleza ni lini alitembelea maeneo hayo mawili, ambayo sasa inasema ni ardhi yake. 

Aidha, ripoti zinasema kiongozi huyo wa Urusi ambaye pia ni amiri jeshi mkuu alitembelea kambi kuu ya jeshi ya Dniepr, iliyo Kherson, Kusini mwa nchi ya Ukraine. 

Inaelezwa kuwa alipokea ripoti kuhusu wakuu wa jeshi kuhusu hali ya usalama huko Kherson na  Zaporizhzhia huku ikibainika kuwa hakuandamana na Waziri wa usalama Sergei Shoigu au Mkuu wa Majeshi Valery Gerasimov. 

Hii ndio mara ya kwanza kwa Putin kutembelea majimbo hayo mawili, ambayo yanadhibitiwa na wanajeshi wa Urusi, tangu kuchukuliwa mwaka uliopita, wakati Moscow ilipoandaa kura ya maoni iliyopingwa na Mataifa ya Magharibi na Ukraine. 

Mykhailo Podolyak, mshauri wa kiongozi wa Ukraine, kupitia ukurasa wake wa Twitter, amechekelea ziara hiyo, akiita matembezi maalum. 

Ukraine na mataifa ya Magharibi, yanaishtumu vikosi vya Urusi kwa kutekeleza uhalifu wa kivita katika maeneo wanayodhibiti , madai ambayo Moscow inakanusha. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.