Pata taarifa kuu

China: Li Qiang, mshirika wa karibu wa Xi Jinping ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Kwa muda wa wiki moja , kikao cha kila mwaka cha bunge kimekuwa kikifanyika. Kikao hiki kinaashiria kuanza kwa mamlaka mpya, ya kipekee kwa Xi Jinping, na kuondoka kwa Waziri Mkuu Li Keqiang, ambaye aliteuliwa kwa wadhifa huu Machi 15, 2013. Huyu ni Li Qiang, rafiki wa karibu wa Xi Jinping, mwanachama wa kamati ya kudumu ya ofisi ya kisiasa ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambaye anamrithi kwenye wadhifa wa waziri mkuu.

Rais Xi Jinping wa China (kushoto) akizungumza na Li Qiang wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Watu wa China, Machi 10, 2023.
Rais Xi Jinping wa China (kushoto) akizungumza na Li Qiang wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Watu wa China, Machi 10, 2023. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Idadi kubwa ya wajumbe takriban elfu 3 ilimpigia kura Li wa umri wa miaka 63 wakati wa mkutano wa wiki moja wa kila mwaka wa bunge hilo, hili likiwa kusanyiko kubwa la chama cha Kikomunsti nchini China. Mwanasiasa huyo mashuhuri anajulikana kuwa mshirika wa karibu wa rais Xi Jinping.

Kabla ya kongamano la mwisho la Chama cha Kikomunisti cha China mwezi Oktoba mwaka jana, watu wachache nje ya China walisikia wakimzungumzia Li Qiang, na walishuku kwamba uenda akawa kiongozi wa pili mwenye nguvu katika vyombo vya dola. Lakini wakati kamati ya kudumu ya ofisi ya kisiasa ya chama ikitangaza, katibu mkuu wa chama huko Shanghai alionekana akiambatana na Xi Jinping. Li Qiang ameteuliwa kwenye wadhifa huu, licha ya ukosoaji mkubwa. Kupandishwa cheo kwa afisa huyu asiye na uzoefu katika ngazi ya serikali kuu ni jambo la kushangaza.

Akiwa na umri wa miaka 63, Li Qiang ni mwanasiasa wa kikazi ambaye alipanda ngazi kama kada wa chama katika jimbo lake la asili, hadi mwaka wa 2005 akawa katibu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha Zhejiang. Wakati huo alikuwa moja kwa moja chini ya maagizo ya Xi Jinping, wakati huo katibu mkuu wa mkoa wa pwani, ambaye alianzisha uhusiano wa karibu naye. Li Qiang alikua gavana wa Zhejiang mwishoni mwa mwaka 2012 kabla ya kupandishwa cheo na kuwa mkuu wa mkoa wa Jiangsu mwaka 2016 ili kuziba ombwe la kisiasa lililosababishwa na kashfa ya ufisadi. Mwaka mmoja baadaye, aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa Shanghai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.