Pata taarifa kuu

Marekani: Kile kinachojulikana kuhusu uharibifu wa puto la China

Beijing inazungumza juu ya "hatua ya utumizi wa nguvu wa kupindukia" baada ya Marekani kuangusha puto lisilokuwa na rubani la China lililokuwa juu ya anga ya Marekani katika siku za hivi karibuni. Hata hivyo Marekani imelitaka puto hilo kuwa la kijasusi. Rais wa Marekani Joe Biden aliwapongeza marubani walioiangusha puto la China na Waziri wake wa Ulinzi alitoa maelezo ya operesheni hiyo.

Ndege ya Marekani ikiharibu puto la China, Februari 4, 2023.
Ndege ya Marekani ikiharibu puto la China, Februari 4, 2023. AP - Chad Fish
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Lloyd Austin, mkuu wa Pentagon, puto la China lilikuwa likijaribu kutazama "maeneo ya kimkakati" nchini Marekani ilipoonekana Alhamisi Februari 2. Ilikuwa inaruka kwa urefu wa juu sana juu ya anga la jimbo la Montana la Marekani na hasa juu ya eneo la makombora ya nyuklia. Jeshi la Marekani liliweza kufuatilia njia ya puto, ambayo iliruka juu ya anga ya Marekani kwa mara ya kwanza huko Alaska Jumamosi Januari 28. Kisha lilionekana nchini Canada siku ya Jumatatu Januari 30, kabla ya kurudi tena kuonekana juu ya anga ya Marekani katika eneo la Idaho, Jumanne Januari 31.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa ndege zake za kivita ziliidondosha puto hiyo kwenye eneo la maji ya Marekani.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani inaelezea kwamba ilitaka kuondoa hatari yoyote kwa watu walio chini. Usafiri wa ndege za kiraia ulikuwa umesimamishwa hapo awali katika viwanja vitatu vya ndege katika majimbo ya Carolina Kaskazini na Kusini kama hatua ya "usalama wa taifa".

Puto la China laharibiwa na F-22

Ndege ya kivita ya Lockheed Martin F-22 Raptor ndiyo iliyopewa jukumu la kuharibu puto la China lililokuwa likiruka kwenye anga ya Marekani, ambalo wakati huo lilikuwa kwenye mwinuko wa kilomita 18. Mara moja ilianza operesheni nyingine maridadi: ile iliyolenga kurejesha mabaki ya chombo hiki ca China kilichoanguka baharini. Na hii ili kujua ni vifaa gani lilikuwa limebeba, lakini pia ni aina gani na kiasi cha habari lilichoweza kukusanya.

"Puto za uchunguzi wa China zilipita kwa muda mfupi juu ya anga ya Marekani angalau mara tatu wakati wa utawala uliopita na mara moja mwanzoni mwa utawala huu, kama tunavyojua," afisa mkuu wa Marekani alisema siku ya Jumamosi.

Kwa upande wake China imeelezea, "kutoridhishwa na kupinga hatua hiyo dhidi ya utumizi wa nguvu wa Marekani kushambulia ndege za kiraia zisizo na rubani", Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema katika taarifa yake na kuongeza kuwa "inahifadhi haki" ya kujibu. Kulingana na taarifa hii, Beijing inaamini kwamba Washington "imepindukia wazi" na "imekiuka sana mazoea ya kimataifa", kulingana na chanzo hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.