Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Xi Jinping achaguliwa kwa muhula wa tatu kuwa rais wa Jamhuri ya Watu wa China

Akiwa madarakani tangu 2013 na kuchaguliwa kama rais kwa mara ya kwanza mwaka 2018, Xi Jinping alichaguliwa tena kwa kauli moja, bila ya kushangaza, kuwa rais wa China Ijumaa Machi 10, katika kura ya wabunge. Ataongoza China kwa muhula wa tatu wa miaka mitano, jambo ambalo halijawahi kutokea nchini humo.

Rais Xi Jinping wa China akipiga makofi wakati wa kikao cha Baraza la Bunge mjini Beijing Machi 10, 2023, siku ambayo alichaguliwa tena kuwa rais kwa muhula wa tatu.
Rais Xi Jinping wa China akipiga makofi wakati wa kikao cha Baraza la Bunge mjini Beijing Machi 10, 2023, siku ambayo alichaguliwa tena kuwa rais kwa muhula wa tatu. AP - Mark Schiefelbein
Matangazo ya kibiashara

Xi Jinping yuko madarakani kwa miaka kumi, na hapa anatarajia tena kuongoza China kwa miaka mingine mitano. Hakukuwa na mashaka yoyote juu yake. Xi Jinping amechaguliwa tena Ijumaa Machi 10 kuwa rais wa China kwa muhula wa tatu, jambo ambalo halijawahi kutokea nchini China, baada ya kura rasmi.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 69 tayari alikuwa amepata nyongeza ya miaka mitano Oktoba 2022 kuwa mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha CCP na mwenyekiti wa tume ya kijeshi, nyadhifa mbili muhimu zaidi za madaraka nchini humo. Kuchaguliwa kwake tena ni kilele cha ongezeko ambalo limemfanya kuwa kiongozi mwenye nguvu zaidi nchini tangu vizazi kadhaa.

Taarifa zaidi za kukujia

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.