Pata taarifa kuu

Ajali ya ndege ya MH17: Watu watatu wahukumiwa kifungo cha maisha nchini Uholanzi

Mahakama ya Uholanzi siku ya Alhamisi (Novemba 17) imewahukumu watu watatu kifungo cha maisha na kumwachilia mwingine kwa kosa la kudungua ndege MH17 ya shirika la ndege la Malaysia Airlines nchini Ukraine mwaka 2014, huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kuhusu uvamizi wa Urusi.

Mahakama hiyo ikiongozwa na Jaji Steenhuis (wa pili kushoto) wakati wa hukumu ya kesi ya watu wanne walioshtakiwa kwa kuhusika katika kesi ya ajali ya ndege MH17, huko Badhoevedorp, Uholanzi, Novemba 17, 2022.
Mahakama hiyo ikiongozwa na Jaji Steenhuis (wa pili kushoto) wakati wa hukumu ya kesi ya watu wanne walioshtakiwa kwa kuhusika katika kesi ya ajali ya ndege MH17, huko Badhoevedorp, Uholanzi, Novemba 17, 2022. AFP - JOHN THYS
Matangazo ya kibiashara

Warusi Igor Girkin na Sergei Dubinsky na raia mmoja wa Ukraine Leonid Kharchenko 'wamepatikana na hatia' ya mauaji na kuhusika katika kuangusha ndege, Mrusi Oleg Poulatov ameachiliwa huru, jaji kiongozi Hendrik Steenhuis amesema. Watatu wa kwanza walipatikana na hatia bila kuwepo mahakamani, kwani wote wanne walikataa kuhudhuria kesi hiyo, iliyochukua miaka miwili na nusu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa upande wake amekaribisha "uamuzi huu muhimu". "Adhabu kwa ukatili wote wa Urusi - jana na leo - haitaepukika," ameongeza.

Ndugu wengi wa wahanga kutoka kote ulimwenguni walisafiri kwenda kusikiliza hukumu kwa kesi hii iliyotarajiwa sana katika mahakama yenye usalama karibu na uwanja wa ndege wa Amsterdam-Schiphol, ambapo Boeing 777 iliruka Julai 17 2014. Upande wa utetezi au wa mashitaka unaweza kukata rufaa.

Ushahidi mwingi unaohusishwa na urushaji wa kombora la BUK

Abiria na wafanyakazi wote 298 walipoteza maisha wakati ndege hiyo kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur ilipodunguliwa mashariki mwa Ukraine, eneo lililokuwa likishikiliwa na watu wanaounga mkono Urusi, na kile waendesha mashtaka wanasema ni kombora lililotolewa na Moscow. Majaji waliamua kwamba Igor Girkinen, Sergei Dubinsky na Leonid Kharchenko wote waliwajibika kwa kusafirisha kombora la BUK kutoka kambi ya kijeshi nchini Urusi na kulipeleka kwenye eneo la tukio, ingawa hawakuhusika peke yao. Hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba Oleg Pulatov, mshukiwa pekee aliwakilishwa na mwanasheria wake wakati wa kesi hiyo, alihusika, wamesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.