Pata taarifa kuu

Ukraine: Volodymyr Zelensky atathmini mashambulizi ya Urusi na anawashukuru wananchi wake

Nchini Ukraine, mapigano yanaendelea hata kama taarifa juu ya kusonga mbele kwa wanajeshi wa Ukraine inazidi kuwa nadra. Mashambulizi ya Urusi pia hayakomi, lakini hayatoshi kuwakatisha tamaa Waukraine kama Rais Volodymyr Zelensky alivyothibitisha tena katika matangazo ya video usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika mkutano kuhusu ujenzi mpya wa Ukraine kwa mwaliko wa Umoja wa Ulaya na G7, Jumanne, Oktoba 25.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika mkutano kuhusu ujenzi mpya wa Ukraine kwa mwaliko wa Umoja wa Ulaya na G7, Jumanne, Oktoba 25. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo sio ya kawaida kwa upande wa Volodymyr Zelensky. Katika video iliyorushwa jana usiku, rais wa Ukraine, ambaye kwa kawaida yake hukaa kwenye kiti nje ya ofisi yake mbele ya mabaki ya ndege isiyo na rubani, akitoa ripoti ya siku mbili zilizopita ambapo ulinzi wa Ukraine umeweza kukabiliana na mashambulizi kadhaa ya Urusi. 

"Siku ya 246 imemalizika. Tunaendelea na upinzani wetu. Mchokozi anaendelea na ugaidi wake. Tunashambuliwa tena kutoka mbinguni na kundi la kunguru wao. Zaidi ya ndege 30 zisizo na rubani zilirushwa ndani ya siku mbili. Watetezi wa anga yetu waliwazuia tai wa adui kupenya nyuma ya nchi na kuangusha Shahed 23 (ndege zisizo na rubani kutoka Iran). Kwa jumla, katika kipindi hiki, Urusi ilifanya mashambulizi 4,500 ya makombora na mashambulizi zaidi ya 8,000 ya anga. Lakini tunapigana, tutapiga zaidi," rais wa Ukraine amesema.

Volodymyr Zelensky anachukua fursa hii kuwashukuru wananchi wake ambao wanapigana bila huruma, pamoja na watu wote walioshiriki katika kukusanya fedha na ambao waliwezesha ununuzi wa vifaa vilivyowezesha uharibifu wa ndege zisizo na rubani. Baada ya wiki za ugaidi, hata huko Kyiv katika siku za hivi karibuni, vikosi vya Ukraine vilionekana kuwa na uwezo wa kukabiliana na mashambulizi ya Urusi, hata kama raia wanakufa kila siku kutokana na mashambulizi ya mabomu ambayo pia husababisha uharibifu mkubwa wa vifaa.

Katika mkoa wa Donetsk, wanajeshi wa Ukraine hawajafanya vizuri na kusini na hasa katika mkoa wa Kherson, askari wa Ukraine wanasonga mbele polepole kuelekea mji mkuu huu wa mkoa ambapo, kulingana na mamlaka ya Urusi, wakazi 70,000 wamehamishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.