Pata taarifa kuu

Putin: Dunia inaingia muongo 'hatari zaidi' tangu 1945

Wakati wa hotuba iliyotolewa Alhamisi hii huko Moscow mbele ya kongamano la majadiliano la Valdaï, rais wa Urusi ametangaza kwamba nchi yake, ambayo ilianzisha vita nchini Ukraine, ilikuwa inatetea tu "haki yake ya kuwepo" dhidi ya madola ya Magharibi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, wa pili kulia, akiambatana na Naibu Kamanda wa Vikosi vya Wanajeshi wa Anga Anatoly Kontsevoy, kulia, kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Wilaya ya Kijeshi ya Magharibi kwa askari wa akiba waliohamasishwa katika Mkoa wa Ryazan, Urusi, Oktoba 20, 2022.
Rais wa Urusi Vladimir Putin, wa pili kulia, akiambatana na Naibu Kamanda wa Vikosi vya Wanajeshi wa Anga Anatoly Kontsevoy, kulia, kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Wilaya ya Kijeshi ya Magharibi kwa askari wa akiba waliohamasishwa katika Mkoa wa Ryazan, Urusi, Oktoba 20, 2022. AP - Mikhail Klimentyev
Matangazo ya kibiashara

"Urusi haipingi nchi za Magharibi, Urusi inatetea tu haki yake ya kuwepo," amesema, akiwashutumu Wamarekani na washirika wao kwa kutaka "kuharibu, kufuta" Shirikisho la Urusi "kutoka kwenye ramani".

Ulimwengu unaingia katika muongo wake "hatari zaidi" tangu Vita vya Pili vya Dunia, Vladimir Putin pia amebainisha, katika mashtaka haya mapya makali dhidi ya nchi za Magharibi.

"Tuko katika wakati wa kihistoria. Bila shaka tunakabiliwa na muongo hatari zaidi, muhimu, usiotabirika” tangu 1945; sayari iko katika "hali ya mapinduzi", kwa sababu nchi za Magharibi "zinatafuta sana" kulazimisha utawala wake.

Nchi za Magharibi zinacheza "mchezo hatari, umwagaji damu na mchafu" katika vita vya Ukraine, lakini hivi karibuni itabidi kuanza mazungumzo na Moscow katika uso wa mgogoro wa kimfumo uliosababishwa na matukio ya ulimwengu katika miezi ya hivi karibuni, Putin amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.