Pata taarifa kuu

Biden: Matumizi ya silaha za nyuklia za Urusi nchini Ukraine yatakuwa na 'athari mbaya'

Urusi inajikuta katika hali tete ya kidiplomasia juu ya vita vya Ukraine, kama vile jeshi lake katika uwanja wa vita. Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye alikuwa akitafuta uungwaji mkono madhubuti katika mkutano wa kilele huko Samarkand, Uzbekistan, alijikuta akikabiliwa na China huku India ikielezea tahadhari na kutochukuwa msimamo wowote. Rais wa Marekani Joe Biden naye ameionya vikali Ikulu ya Kremlin dhidi ya kutumia silaha za kemikali au nyuklia.

Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi jibu "thabiti" ikiwa Urusi itatumia silaha za kemikali au nyuklia nchini Ukraine. Hapa, ilikuwa wakati alipohutubia taifa mnamo Septemba 1, 2022 huko Philadelphia.
Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi jibu "thabiti" ikiwa Urusi itatumia silaha za kemikali au nyuklia nchini Ukraine. Hapa, ilikuwa wakati alipohutubia taifa mnamo Septemba 1, 2022 huko Philadelphia. © AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Hili ni moja ya maswala ya ujasusi wa Marekani kwa miezi kadhaa. Hayo yanadhihirika na hali inayowakabili wanajeshi wa Urusi katika uwanja wa vita nchini Ukaine. Wasiwasi huu ni kwamba Vladimir Putin baada ya kupoteza maeneo kadhaa yaliyokuwa yanadhibitiwa na jeshi lake,  atakuja kufanya matumizi makubwa ya silaha za kemikali au silaha za nyuklia katika vita hivyo vinavyoendelea. Wakati wa kipindi cha kisiasa cha Jumapili kwenye kituo cha CBS "Dakika sitini", Joe Biden alikuwa muwazi, anaripoti mwandishi wetu huko Washington, Guillaume Naudin:

“Usifanye, usifanye, usifanye. Hiyo itabadili sura ya vita kama ambavyo hakuna kilichotokea tangu Vita vya pili vya dunia. "

Akishawishiwa kusema hatua itakayochukuliwa na Marekani ikiwa hilo litatokea, Joe Biden amekataa kujibu kwa usahihi, lakini ametoa jibu akionesha msimamo wa Marekani: "Itakuwa atahari mbaya, na madhara makubwa. Hali itakuwa mbaya zaidi duniani kuliko alivyofiria. Na kulingana na ukubwa wa kile watakachokifanya, tutaamua ni jibu gani litatolewa. »

Kutokana na kusonga mbele kwa wanajeshi wa Ukraine, ambao anawashutumu bila uthibitisho wa kutaka kufanya vitendo vya kigaidi katika nchini Urusi, Vladimir Putin alielezea katika hitimisho la mkutano wa kilele wa Samarkand kwamba majibu ya jeshi lake yanapimwa.

Maliza mzozo "haraka iwezekanavyo"

Na kutokana na msimamo wa India, ambayo ilithibitisha kwamba "wakati sio wa vita", rais wa Urusi alisema alisikia "wasiwasi" wake, akichukua maneno ambayo alikuwa ametumia siku moja iliyopita akimwambia rais Xi Jinping. Rais wa Urusi alimwambia Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwamba "atafanya kilio chini ya uwezo wake" kuhakikisha kwamba mzozo wa Ukraine "unamalizika haraka iwezekanavyo".

Lakini, akiongea baadaye kidogo na vyombo vya habari vya Urusi, mkuu wa Kremlin alitangaza kwamba Moscow haikuwa na haraka ya kukamilisha "lengo lake kuu" nchini Ukraine: ushindi wa Donbass, eneo la kusini-mashariki mwa nchi linalodhibitiwa na jeshi la Urusi. "Mpango (wa operesheni) hauhitaji mabadiliko (...) hatuna haraka," alisema Vladimir Putin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.