Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Armenia: Mlipuko wa bomu wasabisha uharibifu mkubwa Yerevan

Mlipuko wa asili isiyojulikana Jumapili ulisababisha "waathiriwa" katika eneo la kibiashara huko Yerevan, mji mkuu wa Armenia,  mamlaka ya nchi hii ya Caucasia imetangaza

Wanajeshi wa Armenia wakitoa ulinzi kwenye kituo cha ukaguzi, karibu na mpaka na la Azerbaijan.
Wanajeshi wa Armenia wakitoa ulinzi kwenye kituo cha ukaguzi, karibu na mpaka na la Azerbaijan. AFP - KAREN MINASYAN
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulitokea katika soko la jumla la Surmalu. "Kulingana na ripoti ya awali, mlipuko huo ulitokea umesababisha tukio la moto. Kuna majeruhi kadhaa," Wizara ya masuala ya Dharura imesema katika taarifa, na kuongeza kuwa timu za maafisa wa idara ya huduma za dharura zimewasili kwenye eneo la tukio.

Asili ya mlipuko huo, ambao ulitokea mapema alasiri katika soko la jumla la Surmalu, haijulikani.

Video na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi mwingi mweusi ukipanda angani. Kwenye video, unaweza kusikia milio kadhaa mfululizo, kama milipiuko ya fataki.

Kulingana na Wizara ya Hali ya Dharura, magari kumi ya kikosi cha Zima Moto yapo kwenye eneo la tukio na mengine kumi yapo njiani kutoa msaada.

Armenia, nchi ndogo katika Caucasia yenye watu wapatao milioni tatu, imekuwa ikipitia kipindi kigumu tangu vita vya mwaka 2020 dhidi ya taifa jirani la Azerbaijan vilivyomalizika kwa kushindwa vibaya pamoja na mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.