Pata taarifa kuu

Urusi yaishutumu Ukraine kwa 'ugaidi wa nyuklia'

Urusi imefutilia mbali madai ya kuhusika kwake katika mashambulio karibu na kinu cha nyuklia huko Zaporizhia, nchini Ukraine, ikishutumu serikali ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa "ugaidi wa nyuklia". 

Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Rais wa Urusi Vladimir Putin. © MIKHAIL KLIMENTYEV, SPUTNIK VIA AFP
Matangazo ya kibiashara

"Makundi yenye silaha ya Ukraine yamefanya mashambulizi matatu ya silaha dhidi ya eneo la kinu cha nyuklia cha Zaporizhia na jiji la Energodar," jeshi la Urusi limesema katika taarifa, likitoa wito kwa "mashirika ya kimataifa kulaani vitendo vya utawala wa Zelensky ambao hufanya vitendo vya ugaidi wa nyuklia."

Ukraine inasema Urusi imefanya mashambulizi karibu na kinu cha nyuklia huko Zaporizhia, ambayo imekuwa chini ya uvamizi wa Urusi tangu kuanza kwa vita.

Waya zinazosafirisha kiwango kikubwa cha umeme zimeharibiwa katika shambulio hili, na kusababisha kuzimwa kwa moja ya vinu vya kituo cha nguvu, kikubwa zaidi barani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.