Pata taarifa kuu
INDONESIA- USALAMA

Indonesia: Waasi wakiri kuhusika na shambulio katika eneo la Papua

Waasi wanaotaka kujitenga katika eneo la Papua mashariki mwa Indonesia, wamekiri kuhusika na shambulio la wikendi iliyopita ambapo watu 10 waliuawa kwa kudaiwa kuwa majasusi wa serikali jijini Jakarta.

Wakaaji wa Papua wanaotaka kujitenga na Indonesia.
Wakaaji wa Papua wanaotaka kujitenga na Indonesia. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamesema kuwa makundi ya watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki na silaha zengine walivamia lori la wafanyibiashara lilokuwa linasafirisha bidhaa kupitia katika eneo hilo waasi hao wakihusishwa na tukio hilo.

Waasi katika eneo hilo la Papua, ambao kwa miongo kadhaa sasa, wamekuwa wakitekeleza mashambulio dhidi ya vikosi vya serikali, katika siku za hivi karibuni wameonekana kuzidisha mashambulio kwa watu wanaodhaniwa kuwa na uhusiano na serikali.

The West Papua National Liberation Army (TPNPB), kundi la wapiganaji wanaotaka kujitenga, limesema kuwa liliwapiga risasi raia hao kwa sababu liliaamini walikuwa wanatoa taarifa za kijasusi kwa serikali kwa kisingizio kuwa walikuwa ni wafanyibiashara.

Shambulio la Jumamosi limetajwa kuwa mbaya zaidi kutokea katika maika ya hivi karibuni katika jimbo hilo lenye utajiri wa madini.

2018, watu 19 wafanyikazi wa kampuni ya ujenzi inayomilikiwa na serikali waliuawa kwa kupigwa risasi baada ya kushambuliwa na waasi hao walipokuwa wanakarabati daraja.

Mwezi Machi, wafanyikazi 8 wa kampuni moja ya mawasiliano waliuawa kwa kupigwa risasi.

Papua, ilipata uhuru wake 1961 kutoka kwa uholanzi kabla ya jirani yake Indonesia kuichukua miaka miwili baadae.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.