Pata taarifa kuu
BELARUS-WAHAMIAJI

Poland yatumia gesi ya machozi kuwatawanya wahamiaji, Urusi yalaani

Wakati maelfu ya wahamiaji wamekusanyika kwenye mpaka na Belarus, Poland imetumia gesi ya machozi Jumanne kwa kuwatawanya wahamiaji, kitendo ambacho Urusi imeshtumu kuwa ni cha kinyama.

Kwenye mpaka wa Poland na Belarus karibu na Kuznica, Poland mnamo Novemba 15, 2021.
Kwenye mpaka wa Poland na Belarus karibu na Kuznica, Poland mnamo Novemba 15, 2021. AP - Leonid Shcheglov
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya usalama vya Poland vilitumia gesi ya kutoa machozi dhidi ya wahamiaji waliorusha mawe katika kijiji cha Kuznica (Mashariki) kwenye mpaka na Belarus, Wizara ya Ulinzi ya Poland imetangaza Jumanne hii. "Kuznica: wahamiaji wanashambulia askari na maafisa wetu kwa mawe na kujaribu kuharibu ua ili kuingia Poland," wizara ya usaama imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. “Vikosi vyetu vilitumia gesi ya kutoa machozi kukomesha mashambulizi dhidi ya wahamiaji. Mamlaka ya Poland imeongeza kuwa polisi mmoja alijeruhiwa vibaya kwenye mpaka.

Moscow mara moja imeshutumu matumizi ya Poland "yasiyokubalika" ya mizinga ya maji na mabomu ya machozi kuwafukuza wahamiaji wanaotaka kuvuka mpaka wake kutoka Belarus. "Tabia ya upande wa Poland haikubaliki kabisa," Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov amewaambia waandishi wa habari. "Wanakiuka viwango vyote vya kisheria," ameongeza.

Baada ya wiki moja ya mvutano, Brussels na Washington zilitangaza Jumatatu kwamba wanataka kuongeza vikwazo katika siku za zijazo dhidi ya Minsk, ambayo tayari imechukuliwa vikwazo kwa ukandamizaji usio na huruma tangu mwaka 2020 dhidi ya upinzani. Utawala wa Belarus, ambao Umoja wa Mataifa unashutumu kuandaa tangu msimu wa joto kufurika kwa maelfu ya wahamiaji kwenye mipaka ya Poland na Lithuania kulipiza kisasi kwa vikwazo, hata hivyo, imechukua hatua za kwanza za kutuliza mzozo huo. "Jambo kuu leo ​​ni kutetea nchi yetu, watu wetu na kuepuka mapigano," Alexander Lukashenko amesema Jumanne hii, akinukuliwa na shirika la habari la Belta linalomilikiwa na serikali. "Tatizo hili halipaswi kugeuka kuwa makabiliano makali. "

Zaidi ya watu 2,000 wakusanyika

Kauli hizo zinakuja siku moja baada ya mahojiano na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, mafanikio kwa kiongozi huyo wa Belarus, ambaye viongozi wa nchi za Magharibi wamekataa kuzungumza naye tangu kuchaguliwa kwake tena Agosti 2020.

Kwenye mpaka kati ya Poland na Belarus, zaidi ya wahamiaji 2,000 wamekusanyika mbele ya kituo cha mpaka cha Brouzgui (kama kilomita kumi kutoka Kuznica).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.