Pata taarifa kuu

Mgogoro wa wahamiaji: Poland na Belarus zashinikizwa, wahamiaji wakwama mpakani

Wakimbizi elfu kadhaa bado wamekusanyika kwenye mpaka wa upande wa Belarus na hivyo kuangaliana na kikosi cha wanajeshi kilichowekwa na Poland.

Poland imetangaza Jumatano Novemba 10 kwamba imeanzisha msako dhidi ya wahamiaji waliokusanyika kwenye mpaka na kuwakamata zaidi ya watu hamsini.
Poland imetangaza Jumatano Novemba 10 kwamba imeanzisha msako dhidi ya wahamiaji waliokusanyika kwenye mpaka na kuwakamata zaidi ya watu hamsini. Leonid Shcheglov BELTA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi 15,000 wa Poland sasa wametumwa katika eneo hilo. Warsaw imeeleza Jumatano hii, Novemba 10, kuwa imezuia watu kadhaa wakijaribu kuvuka wakati wa usiku.

Waziri wa Ulinzi wa Poland amehakikisha kwamba hakukuwa na visa vingi vya watu kujaribu kuvuka mpaka, kwenye sehemu moja ya mpaka kama ilivyokuwa mwanzoni mwa juma, lakini majaribio ya wakati mmoja ya makundi madogo ya wahamiaji katika maeneo tofauti ya mpaka. Polisi wa Poland wanasema wamewakamata takriban watu 50 wanaotuhumiwa kujaribu kuvuka mpaka kinyume cha sheria.

Wakati wahamiaji wengi zaidi wakihamia Poland, lakini pia Latvia na Lithuania, Warsaw inaishutumu Belarus kwa kutumia nguvu na vitisho vya kimwili kuwazuia wahamiaji kuingia katika ardhi yake. Kwa upande wake, Minsk inalaani ghasia zinazotumiwa na wanajeshi na polisi wa Poland kuwazuia wahamiaji hao kuvuka mpaka.

Kinachotokea, kile ambacho serikali ya Belarus inafanya, inaitwa tu biashara ya binadamu. Wanatumia binadamu, wanaume, wanawake, watoto, ambao wanakusanya kwenye mpaka, wanatishia, kuweka shinikizo kwa Umoja wa Ulaya" , amesema msemaji wa serikali ya Ufaransa Gabriel Attal, akihojiwa na Anthony Lattier.

"Hiki ni ulipizaji kisasi wa Lukashenko"

Kwa hivyo hali inaendelea kuwa ya wasiwasi sana na kwa sasa, kwa upande wa kidiplomasia, hakuna kinachoonekana kubadilika: Brussels inaongeza tishio la vikwazo vipya dhidi ya Belarus, ambayo inahakikisha kupitia sauti ya rais wake Alexander Lukashenko kwamba " haitokubali kujidhalilisha". EU inajaribu kuonyesha azma yake mbele ya Minsk, ameripoti mwandishi wetu wa Brussels, Pierre Benazet.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.