Pata taarifa kuu

Mgogoro wa wahamiaji: Viongozi wa EU wakubaliana kuhusu vikwazo vipya dhidi ya Belarus

Katika mpaka kati ya Poland na Belarus, maelfu ya wahamiaji bado wamekusanyika kujaribu kuvuka mpaka kati ya nchi ya Poland na Bemlarus.

Kwenye mpaka wa Poland na Belarus karibu na Kuznica, Poland mnamo Novemba 15, 2021.
Kwenye mpaka wa Poland na Belarus karibu na Kuznica, Poland mnamo Novemba 15, 2021. AP - Leonid Shcheglov
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu hii, Novemba 15, Umoja wa Ulaya umepiga kura ya vikwazo vipya dhidi ya Belarus na dhidi ya watu na mashirika yanayochangia kumiminika kwa maelfu ya wahamiaji kwenye mpaka wa Poland.

Umoja wa Ulaya utapitisha "katika siku zijazo" vikwazo vipya dhidi ya watu na mashirika yanayochangia kumiminika kwa maelfu ya wahamiaji kwenye mpaka wa Poland, hali iliyosababishwa na Belarus kulingana na nchi za Magharibi, ametangaza Jumatatu Mkuu wa diplomasia wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell. "Tumekubaliana juu ya kupitishwa kwa vikwazo vipya[...]. Itakamilika katika siku zijazo, "amesema baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 27 za Umoja wa Ulaya huko Brussels. Vikwazo hivi vitaathiri "idadi kubwa ya watu" na kampuni, ameongeza bila hata hivyo kutaja idadi ya watu hao au kutaja kampuni hizo. Orodha ya watu na mashirika yaliyoathiriwa na kuzuiwa kwa mali na marufuku ya kusafiri inatarajiwa kukamilishwa katika wiki zijazo.

Orodha ya vikwazo huenda ikajumuisha shirika la ndege la Urusi Aeroflot, ingawa Poland na Lithuania zinamchukulia rais wa Urusi Vladimir Putin kuwa anahusika na mzozo huu wa mpakani. "Putin anaongoza mgogoro huu kisiasa na Lukasjenko, hiyo ni hakika," Waziri wa Mambo ya Nje wa Lithuania Gabrielius Landsbergis amewaambia waandishi wa habari.

Minsk "inafanya kazi kwa bidii" kuwarudisha wahamiaji waliokwama kwenye mpaka katika nchi zao, kwa upande wake rais wa Belarus Alexander Loukachenko, madarakani kwa miaka 30 amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.