Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini yakosoa mazoezi ya pamoja ya jeshi la Korea Kusini na Marekani

Korea Kusini na Marekani zinaweza kukabiliwa na vitisho zaidi vya usalama ikiwa wataendelea na luteka ya kila mwaka ya kijeshi, Kim Yo Jong, dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amesema Jumanne.

Kim Yo Jong,dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
Kim Yo Jong,dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. AFP - JORGE SILVA
Matangazo ya kibiashara

Korea Kusini na Marekani zimeanza mazoezi ya awali Jumanne hii Agosti 10 na zinatarajiwa kufanya mafunzo makubwa zaidi wiki ijayo, shirika la Habari la Yonhap limeripoti, licha ya onyo kutoka Korea Kaskazini, ambayo inadai kwamba mazoezi haya yatakwamisha maendeleo ya uhusiano kati ya Korea mbili.

Mazoezi haya ni "kitendo kisichohitajika na cha kujiangamiza" kinachotishia raia wa Korea Kaskazini na kuongeza mivutano katika rasi ya Korea, Kim Yo Jong amesema katika taarifa iliyorushwa na shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA.

"Marekani na Korea Kusini zitakabiliwa na tishio kubwa zaidi kwa usalama wao ikiwa watapuuza maonyo yetu ya mara kwa mara na kuendelea na mazoezi haya hatari ya vita," amesema.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Martin Meiners, alikataa kujibu kuhusiana na taarifa hiyo ya Korea Kaskazini, akisema itakuwa kinyume na sera ya wizara kutoa maoni juu ya luteka hiyo.

"Mafunzo ya pamoja ni uamuzi wa pande mbili kati ya Korea Kusini na Marekani, na uamuzi wowote utakuwa kwa makubaliano ya pande zote," amesema.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini pia amejizuia kutoa maoni juu ya mazoezi haya ya awali wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumanne, akisema nchi hizo mbili bado zinajadili tarehe, kiwango na mfumo wa mazoezi ya kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.