Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini yaonya: hakuna mawasiliano na Marekani na "sera ya uhasama"

Korea Kaskazini imetangaza leo Alhamisi kwamba itapuuzia mbali majaribio ya kurejesha mawasiliano na Marekani hadi paleWashington itakapoachana na "sera yake ya uhasama" dhidi yake, shirika la habari la la serikali ya Korea Kaskazini, KCNA, limeripoti.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un aendelea kupinga sera za Marekani kuhusu kuanzisha uhusiano na nchi yake.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un aendelea kupinga sera za Marekani kuhusu kuanzisha uhusiano na nchi yake. via REUTERS - KCNA
Matangazo ya kibiashara

 "Hakuna mawasiliano kati ya Marekani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea na hakuna mazungumzo yoyote yanayoweza kufanyika hadi pale Marekani itakapokomesha sera yake ya uhasama dhidi ya DPRK," amesema Choe Son Hui, Naibu Waziri Mkuu mwenye dhamana ya Mambo ya nje, kulingana na KCNA iliyonukuliwa na shirika la habari la Korea Kusini Yonhap.

"Kwa hivyo, tutaendelea katika siku zijazo kupuuzia majaribio kama hayo ya Marekani," Bi Choe ameongeza.

Onyo la Pyongyang limekuja wakati maafisa wakuu wawili wa Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin, wako ziarani Seoul, mji ,kuu wa Kora Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.