Pata taarifa kuu
JAPANI-AFYA

Japan yapanga kubadili sera yenye utata ya wagonjwa kulazwa hospitalini

Waziri wa afya wa Japan amesema Jumatano wiki hii kwamba serikali inaweza kufikiria kugeuza sera mpya yenye utata inayowataka wagonjwa wa COVID-19 wasio na dalili kali za COVID-19 kujiweka karantini badala ya kwenda hospitalini.

Mtu mmoja kati ya watatu wanaopimwa lazima akutwe na virusi vya Corona katika mji mkuu wa Japan.
Mtu mmoja kati ya watatu wanaopimwa lazima akutwe na virusi vya Corona katika mji mkuu wa Japan. REUTERS - KIM KYUNG-HOON
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga alitangaza kwamba wagonjwa tu mahuruti wa COVID-19 (wanaohitaji msaada wa kupumua) au ambao wanaweza kuwa na dalili kali za ugonjwa huo watalazwa hospitalini.

Waziri wa Afya Norihisa Tamura ametetea sera hiyo, akisema kwamba kwa kuwataka wagonjwa wasio na dalili kali za COVID-19 kujitenga, Japan inaweza kuhakikisha kuwa hakuna uhaba wa vitanda katika hospitali mbalimbali kwa watu wanaohitaji uangalizi mkubwa.

"Janga hilo limeingia katika hatua mpya na kama hatutakuwa na vitanda vya kutosha, hatuwezi kupokea wagonjwa zaidi hospitalini," Norihisa Tamura ameliambia Bunge.

"Ikiwa mambo hayataenda kama ilivyopangwa, tunaweza kupitia sera hii," ameongeza,huku akibaini kuwa mabadiliko haya ya sera yanalenga kudhibiti kuenea kwa haraka kwa aina mpya ya kirusi cha Corona, Delta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.