Pata taarifa kuu
BOSNIA-HAKI

Majaji wathibitisha hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya Mladic

Aliyekuwa Kamanda wa Bosnia Ratko Mladic, amepoteza rufaa aliyowasilisha mwaka 2017 kupinga kuhusika ushiriki wake wa mauaji ya kimbari na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kiongozi wa zamani wa jeshi la Bosnia ya Serbia Ratko Mladic akitoa ishara kabla ya hukumu yake ya rufaa mbele ya mahakama ya kimataifa inayofanya kazi zilizosalia za Mahakama ya Jinai (IRMCT) huko Hague, Uholanzi, Juni 8 2021.
Kiongozi wa zamani wa jeshi la Bosnia ya Serbia Ratko Mladic akitoa ishara kabla ya hukumu yake ya rufaa mbele ya mahakama ya kimataifa inayofanya kazi zilizosalia za Mahakama ya Jinai (IRMCT) huko Hague, Uholanzi, Juni 8 2021. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Umoja wa Mataifa ilikuwa imemhukumu maisha jela baada ya kupatikana na kosa la kuagiza kuuawa kwa watu zaidi ya Elfu nane, wengi wanaume na wavulana wakati wa vita vya Bosnia kati ya mwaka 1992-95.

Mladic aliongoza vikosi vilivyohusika na kampeni ya umwagaji damu ikiwemo mauwaji ya Srebrenica ya mwaka 1995 na kuzingirwa kwa mji wa Sarajevo. Alitiwa hatiani mwaka 2017 na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Uamuzi wa leo kuhusu rufaa ya kesi yake umekamilisha kesi za Umoja wa Mataifa za uhalifu uliofanywa katika vita vya Bosnia ambapo watu zaidi ya laki moja waliuawa na mamilioni kuachwa bila makaazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.