Pata taarifa kuu
Uholanzi

Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari Mladic asomewa mashtaka huko The Hague

Mkuu wa Majeshi wa zamani wa Bosnia Jenerali Ratko Mladic yuko kizimbani , The Hague Uholanzi, mbele ya majaji wanaosikiliza kesi za mauaji ya kimbari ya iliyokuwa Yugoslavia.Mladic aliyefikishwa mahakamani mapema juma hili, akitokea Serbia anakabiliwa na mashtaka kumi na moja ya kivita.

Ratko Mladic, mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya nchini Yugoslavia akiwa mahakamani The Hague.
Ratko Mladic, mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya nchini Yugoslavia akiwa mahakamani The Hague. REUTERS/Martin Meissner/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa mashtaka katika mahakama katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya Yugoslavia, amepasha kuwa mahakama hiyo ina ushahidi wa kutosha juu ya jenerali huyo, ya kutumia mamlaka yake kuua wananchi wasio na hatia huko Srebrenica.

Pamoja na mashtaka mengine, Mladic ambaye sasa ni babu wa miaka takriban 70, anatuhumiwa kuua maelfu ya waumini wa dini ya Kiislam nchini huko.

Baada ya kusomewa mashtaka yote, jaji kiongozi katika mahakama hiyo amemrudisha mtuhumiwa huyo kizimbani, mpaka tarehe 4 Julai, mwaka huu, baada ya Mladic kuomba muda zaidi wa kwenda kusoma mashtaka hayo ili kujiridhisha zaidi.

Pamoja na watu wengine, wazazi wa watu waliokufa katika vita hivyo miaka kumi na sita iliyopita, walikuwa mahakamani hapo kushuhudia kila kilichokuwa kikiendelea.

Hatahivyo, wapo baadhi ya watu nchini Serbia, ambao wanaamini kuwa Mladic hana kosa lolote na kimsingi Mladic ni shujaa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.