Pata taarifa kuu
IRAN

Mazungumzo mapya juu ya mpango wa nyuklia wa Iran kufanyika Vienna Jumanne

Wawakilishi wa Iran na nchi zenye nguvu watakutana tena Jumanne huko Vienna kujadili kuhusu mkataba wa mwaka 2015 juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, maafisa wa Iran naUmoja wa Ulaya wamesema baada ya kikao cha mazungumzo kwa nji ya video leo Ijumaa.

Rais wa Iran Hassan Rouhani akizungumza katika kikao cha baraza la mawaziri huko Tehran.
Rais wa Iran Hassan Rouhani akizungumza katika kikao cha baraza la mawaziri huko Tehran. AP
Matangazo ya kibiashara

Iran, China, Urusi, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza - wote waliosaini mkataba wa mwaka 2015, ulioitwa Mpango wa Pamoja wa Utekelezaji - wamejadili kuhusu uwezekano wa kurudi kwa Marekani katika mkataba huo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Abbas Araqchi, mjumbe mkuu katika mazungumzo kwa upande wa Tehran, ameiambia televisheni ya Iran kwamba baada ya mazungumzo yao ya "wazi na ya busara" leo Ijumaa, washiriki wamekubaliana kukutana mmojabaada ya mwengine Jumanne wiki ijayo huko Vienna.

Vyanzo viwili vya kidiplomasia vya Umoja wa Ulaya pia vimethibitisha mkutano huo.

Marekani kurejea katika mkataba wa mwaka 2015 kwa masharti

Hapo jana Alhamisi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price, alisema wako tayari kutafuta njia ya kurudi katika mkataba huo kulingana na ahadi zilizowekwa chini ya shirika linalofuatilia utekelezaji wake JCPOA na kwa kuhakikisha Iran pia inatimiza ahadi zake.

"Marekani inazungumza na washirika kuhusu njia bora zaidi ya kutimiza hilo ikiwemo kupitia misururu ya hatua za mwanzo", amesema Price.

"Tumekuwa tukitafakari njia mbalimbali za kufanya hili, ikiwemo mazungumzo ya moja kwa moja na washirika wetu wa Ulaya." Price ameongeza.

Hivi karibuni rais wa Marekani Joe Biden aliahidi kuirudisha Marekani kwenye mkataba huo, lakini kwa masharti kwamba Tehran ianze kuheshimu ahadi zake ambazo iliancha kutekeleza kama kulipiza kisasi dhidi ya uamuzi wa Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.