Pata taarifa kuu
MYANMAR-UN-MAUAJI

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu mauaji yanayoendelea nchini Myanmar

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa jeshi la Myanmar linashiriki kwenye uhalifu dhidi ya binadamu, baada ya watalaam wake kuripoti kuwa watu zaidi ya 70 wameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama.

Mazishi ya mwandamanaji aliyeuawa baada ya kupigwa risasi na maafisa usalam 11 Mei 2021.
Mazishi ya mwandamanaji aliyeuawa baada ya kupigwa risasi na maafisa usalam 11 Mei 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi, wamekuwa wakiandamana tangu Februari 1, wakishinikiza kuachiliwa kwa kiongozi wao.

Nchi hiyo inaongozwa na wauaji, wanaotekeleza visa vya ukikukwaji wa haki za binadamu,

amesema Andrews akizungumza na Baraza la Haki za binadamu.

Kumekuwa na shinikizo za kidiplomasia kuwataka wakuu wa jehsi nchini humo kuacha kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji.

Waandamanaji zaidi ya 2,000 wanaoshikiza kuachiliwa huru kwa Suu Kyi, wamekamatwa tangu mwezi Februari.

Jeshi limekuwa likisema chama cha Suu Kyi, cha NLD kiliiba kura wakati wa uchaguzi wa wabunge mwezi Novemba mwaka 2020.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.