Pata taarifa kuu
MYANMAR-ASEAN-SIASA-USALAMA

Mawaziri kutoka nchi wanachama wa ASEAN kuijadili Myanmar

Mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN wanatarajia leo Jumanne kufanya mkutano maalum kuizungumzia hali nchini Myanmar.

Vikosi vya Myanmar vinaendelea kukabiliana na waandamanaji wanaopinga utawala wa kijeshi baada ya kumpindua kiongozi wao Aung San Suu Kyi ambaye amezuiliwa pasipojulikana.
Vikosi vya Myanmar vinaendelea kukabiliana na waandamanaji wanaopinga utawala wa kijeshi baada ya kumpindua kiongozi wao Aung San Suu Kyi ambaye amezuiliwa pasipojulikana. Sai Aung Main AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore, Vivian Balakrishnan ametoa wito wa kuachiwa mara moja kwa kiongozi aliyepinduliwa Aung San Suu Kyi. Balakrishnan amesema mkutano huo utafanyika kwa njia ya video na utawasikiliza wawakilishi wa utawala wa kijeshi nchini Myanmar.

Waziri huyo pia amewataka viongozi wa kijeshi kuacha kutumia nguvu na kuchukua haraka hatua ya kuzuia umwagaji damu, ghasia na vifo. Pia amezitaka pande zote nchini Myanmar kufanya mazungumzo na kutafuta suluhisho la kisiasa la muda mrefu, ikiwemo kutafuta namna ya kurudi katika njia ya mpito ya kidemokrasia.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia amesema jumuia hiyo inapaswa kuchukua jukumu kubwa kurudisha hali ya kawaida Myanmar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.