Pata taarifa kuu
BURMA

Jumuiya ya kimataifa yaonya juu ya mapinduzi Burma

Zaidi ya balozi kumi na mbili, pamoja na ile ya Marekani na ujumbe wa Umoja wa Ulaya, leo Ijumaa wameitaka Burma "kufuata viwango vya kidemokrasia", kwa kujiunga na Umoja wa Mataifa baada ya hali ya wasiwasi kuhusu uwezekano wa mapinduzi katika nchi hiyo.

Aung San Suu Kyi , kiongozi wa kiraia nchini Burma au Mynmar
Aung San Suu Kyi , kiongozi wa kiraia nchini Burma au Mynmar AFP
Matangazo ya kibiashara

Burma iliondoka miaka 10 tu iliyopita katika utawala wa kijeshi ulioshikilia madaraka kwa karibu nusu karne. Katiba, iliyoundwa na kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi wakati huo, inabaini kwamba raia na maafisa wa juu katika jeshi wanatakiwa kuwana madaraka .

Kwa wiki kadhaa, jeshi lenye nguvu nchini humo limeendelea kustumu kuwepo na udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliyofanyika mwezi Novemba 2020, ambapo Chama cha NLD cha Aung San Suu Kyi madarakani kiliibuka mshindi.

Jeshi limeendelea kuomba likisisitiza kuweza kuangalia orodha za uchaguzi, ombi lililoungwa mkono na msemaji wa jeshi Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo hakuficha nia ya jeshi kuchukua nchi ili kukabiliana na kile alichokiita mzozo wa kisiasa.

Hofu iliongezeka zaidi Jumatano wiki baada ya Mkuu wa jeshi Jenerali Min Aung Hlaing - mtu mwenye mwenye ushawishi mkubwa nchini Burma - aliposema katiba ya nchi hiyo inaweza "kubatilishwa" kufuatia hali inayojiri.

Ubalozi wa Marekani - na nchi 16, ikiwa ni pamoja na Uingereza iliyoitawala nchi hiyo katika enzi za ukoloni na ujumbe wa Umoja wa Ulaya -wametoa taarifa leo Ijumaa wakiwataka wanajeshi "kuzingatia viwango vya kidemokrasia".

"Tunatarajia mkutano wa amani wa Bunge mnamo Februari 1, na uchaguzi wa spika, na wakuu wa taasisi hizo mbili ," nchi hizo zimesema katika taarifa ya pamoja.

"(Tunapinga) jaribio lolote la kubadilisha matokeo ya uchaguzi au kuzuia mabadiliko ya kidemokrasia nchini Burma," zimeongeza katika taarifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pia ameelezea "wasiwasi mkubwa" juu ya hali ya hivi karibuni nchini Burma, msemaji wake Stéphane Dujarric amesema katika taarifa.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.