Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA-HAKI

Uturuki: Watu karibu 170 walengwa na waranti kwa madai ya uhusiano na Gülen

Watu wengi wamekamatwa Jumanne hii na polisi wa Uturuki kama sehemu ya operesheni kubwa iliyolenga watu 167, wengi wao wakiwa wanajeshi, wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na mhubiri aliyekimbilia uhamishoni Fethullah Gülen, televisheni ya serikali imeripoti.

Mhubiri wa Uturuki Fethullah Gülen, ambaye sasa yuko uhamishoni nchini Marekani, hapa ilikuwa Julai 10, 2017 nyumbani kwake huko Pennsylvania.
Mhubiri wa Uturuki Fethullah Gülen, ambaye sasa yuko uhamishoni nchini Marekani, hapa ilikuwa Julai 10, 2017 nyumbani kwake huko Pennsylvania. REUTERS/Charles Mostoller
Matangazo ya kibiashara

Gülen, ambaye anaishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka 1999, anatuhumiwa kupanga mapinduzi yaliyotibuliwa mwezi Julai 2016 dhidi ya rais Recep Tayyip Erdogan.

Operesheni mbalimbali zinandeshwa tangu mapema ausubuhi. Ya kwanza imezinduliwa katika mkoa wa pwani wa Izmir na inalenga watuhumiwa 110 katika zaidi ya mikoa 20, kulingana na kituo cha TRT Haber, ambacho kinaripoti watu 89 wamekatwa kufikia sasa.

Operesheni ya pili inalenga watu 57 wanaoshukiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Gülen katika mikoa kumi na tano, linasema shirika la habari la Anadolu.

Tangu jaribio la mapinduzi la mwezi Julai 2016, jaribio ambalo Gülen anakanusha kuhusika, watu wengine elfu 80 wanazuiliwa na karibu wafanyakazi wa serikali 150,000 wamefukuzwa au kusimamishwa kazi katika sekta Elimu, jeshi na katika sekta nyingine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.