Pata taarifa kuu
UJERUMANI-NAVALNY-AFYA-SIASA

Madaktari wa Omsk: Tumeokoa maisha ya Alexeï Navalny

Madaktari katika hospitali ya Siberian ambao walimtunza Alexeï Navalny, kiongozi wa upinzani wa Urusi, wamebaini kwamba wameokoa maisha yake, lakini wamesema hawakupata dalili yoyote sumu.

Alexeï Navalny, kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkuu wa rais wa Urusi Vladimir Putin.
Alexeï Navalny, kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkuu wa rais wa Urusi Vladimir Putin. Mladen ANTONOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Alexeï Navalny alilazwa hospitalini huko Omsk Alhamisi wiki iliyopita baada ya kuwa katika hali ya mahututi kisha kusafirishwa na ndege hadi nchini Ujerumani siku ya Jumamosi. Wafuasi wake walikuwa na hofu kuwa alipewa sumu.

"Tumeokoa maisha yake baada ya kufanya kazi kwa bidii iliyotuchukuwa muda mrefu," Afisa Mkuu wa Matibabu Alexander Murakhovsky amesema wakati mkutano huko Omsk.

"Kama tungekuwa tumeona dalili ya sumu, ingekuwa rahisi zaidi kwetu", ameaongeza Anatoly Kalinichenko, daktari mwingine katika hospitali hiyo.

Timu ya matabibu pia imehakikisha kwamba hawakupata shinikizo lolote kutoka kwa mamlaka.Kulingana na mmoja wa wafuasi wake, maisha ya Alexeï Navalny hayako tena hatarini.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.