Pata taarifa kuu
URUSI-UJERUMANI-USALAMA-SIASA

Mpinzani wa Urusi Alexei Navalny asafirishwa Berlin

Mpinzani mkuu nchini Urusi na mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin, Alexeï Navalny, amesafirishwa nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuwa katika hali mahututi kwa siku kadhaa katika hosptali moja mnjini Moscow, nchini Urusi.

Ndege iliyobeba mpinzani wa Urusi Alexeï Navalny kwenda Ujerumani iliondoka Jumamosi hii asubuhi kutoka uwanja wa ndege wa Omsk.
Ndege iliyobeba mpinzani wa Urusi Alexeï Navalny kwenda Ujerumani iliondoka Jumamosi hii asubuhi kutoka uwanja wa ndege wa Omsk. Dimitar DILKOFF / AFP
Matangazo ya kibiashara

Alexeï Navalny ataendelea kupata huduma ya matibabu katika hospitali moja maarufu mjini Berlin.

Kusafirishwa huku kunakuja siku kadhaa baada ya mvutano kati ya familia yake na madaktari wa Urusi kuhusu kusafirishwa kwake.

Inaarifiwa kwamba madaktari wa Ujerumani walipowasili kwa ndege iliyokuwa na vifaa vya hali ya juu vya matibabu kutokana na ombi la familia yake, madaktari waliokuwa wanamshughulikia huko Urusi walisema kwamba alikuwa mgonjwa mno na hakuweza kusafiri. Wafuasi wake wanasema hiyo ilikuwa mbinu ya serikali kuhakikisha kwamba anawekwa nchini humo kwa kipindi kirefu hadi pale sumu aliyokuwa amekunywa ipotee mwilini.

Madaktari hao walikubali kuondolewa hospitalini humo kwa mwanasiasa huyo pale shirika linalofadhili usafiri wa Navalny kusema kuwa madaktari wa Ujerumani wamemchunguza na kuona kwamba yuko katika hali anayoweza kusafirishwa. Baada ya hapo daktari mkuu wa hospitali hiyo ya Omsk Anatoly Kalinichenko akawaambia waandishi wa habari kwamba hali yake imeimarika na kwamba familia yake imeamua asafirishwe licha ya hatari zilizoko.

Ikulu ya Kremlin imekanusha kwamba ajizi hiyo ya kusafirishwa kwa Navalny ilikuwa ni mbinu ya kisiasa huku msemaji Dmitry Peskov akisema ulikuwa ni uamuzi wa kimatibabu.

"Asante kwa uvumilivu wenu. Bila msaada wenu, hatungeweza kufika hapa! ", mke wa mpinzani huyo, Yulia Navalnaïa, ambaye anaandamana naye nchini Ujerumani ameandika kwenye Instagram.

"Alexeï anasafirishwa kwenda Berlin. Asanteni sana kwa msaada wenu. Mapambano kwa maisha na afya ya Alexei yameanza sasa, na bado kuna mengi ya kuyapitia, lakini sasa hatua ndogo imepigwa, "msemaji wa Alexeï Navalny, Kira Iarmych amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.