Pata taarifa kuu
INDONESIA-AJALI

Watu 188 wafariki dunia katika ajali ya ndege Indonesia

Ndege ya abiria ya Indonesia, inahofiwa kuanguka mapema asubuhi hii ikiwa na abiria 188. Ndege hiyo ya shirika la Lion Air aina ya Boeing 737 imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege mjini Jakarta, kwa mujibu wa maafisa wa Indonesia.

Tovuti ya kufuatilia safari za ndege ya Flightradar24 inasema ndege hiyo iliwasilishwa kwa Lion Air mwezi Agosti.
Tovuti ya kufuatilia safari za ndege ya Flightradar24 inasema ndege hiyo iliwasilishwa kwa Lion Air mwezi Agosti. Flightradar24/twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Uchukuzi nchini humo imethibutsiha kutoweka kwa ndege hiyo, muda mfupi baada ya kupaa.

Ripoti zinasema kuwa, ndege hiyo ilikuwa inatokea jijini Jakarta, kwenda katika mji wa Pangkal Pinang katika visiwa vya Bangka Belitung.

Kwa mujibu wa chanzo cha safari za anga nchini Indonesia ndege hiyo iitoweka kutoka kwenye mitambo ya rada saa kadha baada ya kupaa, ilipokuwa inavuka bahari ya Java.

Ndege hiyo mpya aina ya Boeing 737 MAX 8, ilikuwa imewabeba abiria 178 watu wazima, watoto watatu, marubani wawili na wahudumu watano wa ndege, kwa mujibu wa maafisa katika mkutano na waandishi wa habari.

Bado haijajulikana chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo kwa mujibu wa mamlaka ya uwanja wa ndege wa Jakarta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.