Pata taarifa kuu
CHINA-HONG KONG-HAKI

Edward Leung ahukumiwa kifungo cha miaka sita jela

Kiongozi wa wanaharakati ambao wamekuwa wakishinikiza kwa Hong Kong kutoka China, Edward Leung, amehukumiwa jela miaka sita. China imeenelea kuonya nchi yoyote ile kulitambua eneo la Hongo Kong kama taifa huru.

Edward Leung, alifunguliwa mashitaka kwa kuandaa maandamano ya kushinikiza Hong Kong kujitenga na kujitegemea
Edward Leung, alifunguliwa mashitaka kwa kuandaa maandamano ya kushinikiza Hong Kong kujitenga na kujitegemea REUTERS/Bobby Yip
Matangazo ya kibiashara

Mwaka 2016, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 27, alifunguliwa mashitaka kwa kuandaa maandamano ya kushinikiza Hong Kong kujitenga na kujitegemea.

Aidha, amepewa kifungo cha mwaka mmoja, baada ya kupatikana na kosa la kumjeruhi afisa wa polisi wakati wa makabiliano na maafisa wa usalama mwaka 2016.

Vurugu hizo, ambazo ni mbaya zaidi kuwahi kutokea Hong Kong tangu miongo kadhaa iliyopita, zilisababisha watu zaidi ya 120 kujeruhiwa ambapo waandamanaji wakijihami kwa mawe walikabiliana na vikosi vya usalama katika kata ya Mong Kong.

Karibu watu 130 walijeruhiwa ikiwa ni pamoja na maafisa polisi 90.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.