Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-HAKI

Waendesha mashitaka: Park atakiwa kupewa adhabu kali

Ofisi ya mwendesha mashitaka wa Korea Kusini Jumatano wiki hii amekata rufaa kwa hukumu dhidi ya rais wa zamani wa wa nchi hiyo Park Geun-hye, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 24, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Korea Kusini.

Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye, wakati kesi yake ikianza kusikilizwa huko Seoul Mei 23, 2017.
Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye, wakati kesi yake ikianza kusikilizwa huko Seoul Mei 23, 2017. REUTERS/Ahn Young-joon/Pool
Matangazo ya kibiashara

Waendesha mashitaka walitoa mashitaka 18 yanayomkabiliwa Park Geun-hye na kuomba hukumu ya miaka 30 jela na faini ya ya Wons bilioni 118.5 (sawa na Euro milioni 90). Hata hivyo, aliondolewa makosa mawili na akahukumiwa kifungo cha miaka 24 na faini ya Wons bilioni 18 (sawa na Euro milioni 14). Hukumu hiyo ilitolewa siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita kwa kuhusika kwake katika kashfa kubwa ya ushawishi wa kimadaraka.

Waendesha mashitaka wanbaini kwamba rais wa zamani, ambaye alichaguliwa mwaka 2012, aliondolea makosa hayo mawili kimakosa.

Waendesha mashitaka wanataka hukumu hiyo iongezwe ili iwe mfano kwa viongozi wengine.

Ofisi ya mwendesha mashitaka ya Seoul imesema kuwa hukumu kuhusu mashtaka ya rushwa si halali, " shirika la habari la Korea Kusini Yonhap limearifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.