Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-HAKI

Rais wa zamani wa Korea Kusini afikishwa mahakamani

Aliyekuwa rais wa Korea Kusini, Park Geun-Hye amefikishwa mahakamani kuanza kesi inayomkabili. Hii ni kwa mara ya kwanza aliye kuwa rais wa nchi hiyo kufikishwa mahakamni mjini Seoul kwa tuhuma za ufisadi.

Aliyekuwa rais wa Korea Kusini Park Geun-hye, kuanza kwa kesi yake katika mji wa Seoul, Mei 23, 2017.
Aliyekuwa rais wa Korea Kusini Park Geun-hye, kuanza kwa kesi yake katika mji wa Seoul, Mei 23, 2017. REUTERS/Ahn Young-joon/Pool
Matangazo ya kibiashara

Pia ni kwa mara ya kwanza Park Geun-Hye kuonekana hadharani tangu kuondolewa mamlakani na kuzuiliwa mwezi Machi mwaka huu.

Hata hivyo Park Geun-Hye amekanusha kufanya makosa yeyote, licha ya tuhuma za ufisadi dhidi ya yake.

Bi Park alifika mahakamani akiongozana na rafiki wake wa karibu, Choi Soon-Sil ambae anatuhumiwa kwa kujipatia fedha kutoka kwa makampuni makubwa.
Park Guen-Hye aliulizwa ajira yake na kujibu hajaajiriwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.