Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Ayatollah Ali Khamenei awashtumu maadui wa Iran kuchochea vurugu

Kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amewalaumu maadui wa nchi hiyo kwa kuchochea maadamanio dhidi ya serikali yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo

Kiongozi Mkuu Ali Khamenei mnamo Januari 2, 2018 amewashtumu "maadui wa Iran kuchochea vurugu zinazoendelea nchini Iran.
Kiongozi Mkuu Ali Khamenei mnamo Januari 2, 2018 amewashtumu "maadui wa Iran kuchochea vurugu zinazoendelea nchini Iran. HO / IRANIAN SUPREME LEADER'S WEBSITE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ambayo yanaelekea kumaliza wiki moja sasa yamesababisha vifo vya waandamanaji zaidi ya 20 na mamia kukamatwa katika makabiliano na maafisa wa usalama.

Watu tisa waliuawa usiku wa Jumatatu kuamkia leo Jumanne wakati wa maandamano ya kuipinga serikali katika jimbo la Isfahan katikati mwa Iran, televisheni ya serikali imeripoti leo Jumanne.

Kwa jumla, zaidi ya watu 21 wameuawa tangu kuanza kwa maandamano hayo tarehe 28 Desemba 2017 , kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali. Siku ya Jumatatu, Januari 1, 2018, afisa wa polisi aliuawa wakati wa vurugu zinazohusiana na maandamano ya kuipinga serikali.

Waandamanaji wanalalamikia kupanda kwa gharama ya maisha, na kuzorota kwa uchumi.

Marekani imetangaza kuunga mkono maandamano hayo, huku rais Donald Trump akisema, mabadiliko yanakuja nchini Iran.

Rais Rouhani amemwita rais wa Marekani adui wa taifa lake, ambaye lengo lake ni kuchochea vurugu kwa minajili ya kuuangusha utawala uliopo.

Hayo yakijiri jeshi la mapinduzi nchini humo limeonya kuwa litatumia nguvu dhidi ya waaandamanaji wa upinzani wanaoendelea kujitokeza katika miji mbalimbali.

Mkuu wa jeshi hilo ameonya kuwa, waandamanaji sasa wameanza kuimba nyimbo za kisiasa wakichoma moto mali ya umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.