Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Polisi auawa Iran, rais Rouhani azungumza

Hali ya sintofahamu inaendelea nchini Iran siku tano baada ya kuzuka kwa maandamano. Siku ya Jumatatu, Januari 1, 2018, afisa wa polisi aliuawa wakati wa vurugu zinazohusiana na maandamano ya kuipinga serikali. Watu wasiopungua 13 wamepoteza maisha tangu kuzuka kwa maandamano hayo tarehe 28 Desemba2017.

Moja ya jengo la serikali likichomwa moto na waandamanaji, Doroud, magharibi mwa Iran.
Moja ya jengo la serikali likichomwa moto na waandamanaji, Doroud, magharibi mwa Iran. IRINN/ReutersTV
Matangazo ya kibiashara

Nyimbo dhidi ya serikali bado zinaendelea kusikika katika mitaa ya Tehran. Jumatatu jioni Januari 1, 2018, uwepo wa polisi katika mitaa mbalimbali haujabadilisha chochote. Makundi kadhaa ya waandamanaji yameendelea kukusanyika katikati ya mji mkuu, Tehran.

Mamlaka imeanza kushambulia viongozi wa maandamano hayo. Polisi imewakamata watu kadhaa. Video zilizorushwa kwenye mitandao ya vyombo vya habari vya Iran na mitandao ya kijamii zimethibitisha matukio hayo.

Hassan Rouhani alaani wanaoendesha vurugu Iran

Rais Hassan Rouhani amelaani vurugu zinazoendelea na saa chache baada ya polisi mmoja kuuawa katika mji wa Najafabad, katika mwa nchi. Rais Rouhani amesema serikali yake imeamua "kutatua matatizo ya wananchi," hasa ukosefu wa ajira.

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump amewapongeza waandamanaji nchini Iran akisema kuwa wanapaswa kuungwa mkono. Rais Rouhani amemwita rais wa Marekani adui wa taifa lake, ambaye lengo lake ni kuchochea vurugu kwa minajili ya kuuangusha utawala uliopo.

Hayo yakijiri jeshi la mapinduzi nchini humo limeonya kuwa litatumia nguvu dhidi ya waaandamanaji wa upinzani wanaoendelea kujitokeza katika miji

Mkuu wa jeshi hilo ameonya kuwa, waandamanaji sasa wameanza kuimba nyimbo za kisiasa wakichoma moto mali ya umma.

Tayari watu wawili wameuawa na wengine kukamatwa katika makabiliano na polisi huku mtandao wa Intenetiukikatwa na kuzuia mawasiliano ya simu kupitia mitandao ya kijamii.

Haya ndio maanndamano makubwa kuwahi kushuhudiwa nchii Iran tangu mwaka 2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.